Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akilakiwa na wananchi wa kijiji cha
Damai Kondoa alipowasili kijijini hapo Januari 13,2015 kuzindua msimu wa
kilimo Mkoa wa Dodoma.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaelezea wananchi wa kijiji cha Damai
Kondoa malengo ya kuzindua msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma
Januari 13,2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaelekeza wakina mama wa kijiji cha
Damai Kondoa namna bora ya kupanda kwa nafasi wakati wa uzinduzi wa
msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Chiku Gallawa akiwaonesha kwa vitedo wananchi wa
kijiji cha Damai Kondoa namna bora ya kupanda mazao kwa mstari na nafasi
wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari
13,2015.
Wananchi
wa kijiji cha Damai Kondoa wakshiriki zoezi la kupanda mahindi kwa
mstari na nafasi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani
Dodoma Januari 13,2015.
Mhe.
Chiku Gallawa pamoja na baadhi ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma
wakiwaonesha kwa vitedo wananchi wa kijiji cha Damai Kondoa namna bora
ya kupanda mazao kwa mstari na nafasi wakati wa uzinduzi wa msimu wa
kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mhe.
Chiku Gallawa akiteta jambo na vijana Ramadhani Ismail (kushoto) na
Shafii Ayoub wa kijiji cha Damai Kondoa waliojitokeza kushuhudia
uzinduzi wa msimu wa kilimo mwaka 2015 Mkoani Dodoma Januari 13,2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa amewataka wananchi wa Mkoa wa
Dodoma wale wenye tabia ya kuombaomba chakula cha msaada kuachana na
tabia hiyo mara moja kwani ni aibu kwa kaya zenye tabia hiyo, wilaya na
Mkoa kwa ujumla ukizingatia fursa za kuzalisha chakula cha kutosha
kujikimu mwaka mzima na kuzalisha ziada kwa ajili ya kujiongezea kipato
ipo.
Ili
kufanikisha azma hiyo Mhe. Chiku Gallawa amewataka wananchi wa Dodoma
kuendesha shughuli za kilimo kwa kufuata kanuni za kilimo bora ikiwa ni
pamoja na kuandaa mashamba mapema, kutifua mashamba, kuwahi kupada
mwanzoni mwa msimu wa mvua, kupanda kwa nafasi inayostahili, kuzingatia
matumizi ya mbegu bora, matumizi ya mbolea za viwandani au za wamyama,
kufaya palizi na kulima kwa kuweka makinga maji maneo ya miteremko ama
milima.
Hayo
ameyasema mwanzoni mwa wiki (Januari 13, 2015) Wilayani Kondoa alipokuwa
akizindua msimu wa kilimo kwa mwaka 2015 katika Mkoa wa Dodoma ambapo
aliwataka wananchi kutambua msimu wa kilimo umeanza wananchi wajikite
kwenye kufanya kilimo bora, pia watumie taarifa za utabiri wa hali ya
hewa kujua hali ya upatikanaji wa mvua.
Mhe.
Gallawa akiwa ameambatana na baadhi ya wakuu wa Wilaya za Mkoa wa
Dodoma, viongozi wa Halmashauri zote za wilaya Mkoa wa Dodoma wataalamu
wa kilimo kutoka wilaya zote Mkoani humo walitumia zoezi hilo la
uzinduzi wa msimu wa kilimo kuwaonesha kwa vitendo wanachi wa kijiji cha
Damai Kondoa namna bora ya kulima kwa kufuata kanuni za kilimo bora
kama kutumia mbolea, kupanda kwa nafasi na matumizi ya mbegu bora.
Mhe
Gallawa alitumia nafasi hiyo pia kuwaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri za
Wilaya za Dodoma kuhakikisha kwenye kila kijiji kunakuwa na Daftari la
Kilimo na Mifugo ambalo litakua linatunza taarifa muhimu za shughuli za
kilimo na mifugo zinazofanywa na wananchi vijijini na kutaka wataalam
kilimo na mifugo kuyasimamia kwa umakini. Vlevile alikemea vikali tabia
ya wataalam kujazana ofisini badala ya kutoka kwenda vijijini kwa
wananchi kutoa huduma za kitaalamu.
Akijibu
hoja ya changamoto ya soko la mazao wanayozalisha wananchi wa Dodoma
Mhe. Gallawa amewataka wataalamu wa serikali ya Mkoa na Wilaya wa
masuala ya biashara, Kilimo, ushirika na masoko wawe wanakaa mapema
kabla ya msimu wa kilimo kuanza ili watafute masoko ikiwezekana hata
utaratibu wa kilimo cha mkataba na kuwaelekeza wakulima mazao ya kulima
kabla hata ya msimu.
Kwa
upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Rehema Madenge alibainisha
kuwa zoezi hilo la uzinduzi wa Msimu wa Kilimo Kimkoa limeshafanyika kwa
miaka mitatu mfululizo kweye wilaya za Kongwa, Chamwno na Bahi na
malengo yake ni kuhamasisha wananchi kanuni za kilimo bora.
Mshauri
wa kilimo mkoa wa Dodoma Bw. Bernard Abraham ameelezea kilimo katika
mkoa wa Dodoma kuwa kinaumhimu wapekee kwani asilimia 75% hadi 80% ya
wakazi wa Dodoma ni wakulima wakati ukienda maeneo ya vijiji vya Dodoma
karibu wakazi wake wote wanategemea kilimo kuendesha maisha yao. Mbali
na mkakati huo wa kufanya uzinduzi Rasmi wa Kilimo, ameahidi yeye na
wataalamu wenzie wa kilimo wataendelea kubuni mikakati zaidi ya
kunyanyua kilimo Mkoani Dodoma.
No comments:
Post a Comment