Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimvisha cheo cha
Sajin wa Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa, CPL. Catherina
Lange(hivi sasa cheo cha sajin) wa Gereza Kuu Arusha ambaye ambaye
hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo
kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla. hafla hiyo
imefanyika Januari 13, 2015 katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la
Magereza, Jijini Da res Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akimpongeza Sajin wa
Magereza, Askari Mwanariadha wa Kimataifa, wa Gereza Kuu Arusha mara
baada ya hafla rasmi ya kumvalisha cheo hicho ambapo askari huyo
hushiriki mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo
kuliletea sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(Meza kuu) akitoa
maelezo mafupi kwa Waandishi wa Habari(hawapo pichani) namna Askari
Mwanariadha wa Kimataifa, CPL. Catherina Lange(hivi sasa cheo cha
sajin) wa Gereza Kuu Arusha alivyoshiriki kwa mafanikio makubwa katika
mashindano mbalimbali ya riadha ya Kitaifa na Kimataifa hivyo kuliletea
sifa Jeshi la Magereza na Taifa kwa ujumla.
Wanahabari
toka Vyombo mbalimbali vya Habari wakifanya mahojiano Maalum na Askari
Mwanariadha wa Kimataifa, Sajin wa Magereza Catherina Lange(hayupo
pichani) wa Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo
katika Ofisi za Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe akimpa pongezi Askari
Mwanariadha wa Kimataifa, Sajin wa Magereza Catherina Lange(kulia) wa
Gereza Kuu Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za
Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam.
Mkuu
wa Magereza Mkoani Arusha, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Hamis Nkubas akiwa katika picha ya pamoja na Askari Mwanariadha wa
Kimataifa, Sajin wa Magereza Catherina Lange(katikati) wa Gereza Kuu
Arusha mara baada ya hafla ya uvishaji cheo katika Ofisi za Makao Makuu
ya Jeshi la Magereza, Jijini Da res Salaam(kushoto) ni Mkuu wa Gereza
Kuu Arusha, Themistocles Ifunya.(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la
Magereza).
No comments:
Post a Comment