Na Mwandishi Wetu
MBUNGE wa Viti Maalum
wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Vijana , Mkoa wa Arusha Catherine Magige leo amezindua rasmi duka
jipya la vipodozi na vitu mbalimbali linalofahamika kwa jina la ZuRii
lililopo katika jengo la Dar Free Market lililopo katika barabara ya Alli
Hassan Mwinyi Jijini Dar es Salaam.
Akizindua duka hilo
ambalo linamilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina
George, Magige alisema kwamba amevutiwa na namna Jestina alivyoweza kurudi na
kuwekeza nyumbani hali ambayo imeweza
kuzalisha ajira kwa watanzania na kuwa mfano wa kuigwa.
“Kabla ya yote nachukua
fursa hii kumpongeza Jestina kwani ameonesha mfano
wa umuhimu wa kujiajiri hasa kwa wanawake pia huu ni mfano wa
kuigwa kwa wanadiaspora , wengine warudi
na kuja kuwekeza nyumbani kwani fursa nyingi zipo hivyo waje wazitumie” alisema
Magige.
Aidha alitoa rai kwa
wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na mitaji ya kuanzisha
biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine
pia natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja
kutoa sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati huohuo mmiliki
wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema
kwamba yeye ameona fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.
“Natoa wito kwa kwa wanadiaspora
wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza
kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi hivyo haya
ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu
kwa kutimiza ndoto hii”.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe katika ufunguzi wa ZuRii House of Beauty duka jipya na la kisasa la vipodozi lililofunguliwa rasmi leo Jumatatu 12 Jan 2015 kulia ni Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George.
Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akifungua duka rasmi
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kwa Mgeni rasmi Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige kuhusu bidhaa zilizopo kwenye duka la ZuRii Fashion & Beauty Boutique
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akizungumza na vyombo vya habari kwenye ufunguzi wa duka hilo la vipodozi
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliofika kufanya manunuzi ndani ya duka hilo
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George( kulia) akiwa na mwana harakati mwenzake Shamim Mwasha mmiliki wa blog ya 8020 fashions.
Mkurugenzi wa ZuRii Fashion & Beauty Boutique, Jestina George akitoa ufafanuzi kuhusu ufunguzi na ujio wa duka hilo hapa nchini Tanzania likiwa na muonekano tofauti
Mmoja wa wateja waliofika katika duka hilo akitizama bidhaa
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Catherine Magige (kushoto)
akiwasili kuzindua rasmi duka la urembo la ZuRii House of Beauty
linalomilikiwa na mwana Diaspora ambaye pia ni mwanalibeneke Jestina
George Meru (kulia) ndani ya jengo la Dar Free Market jijini Dar es
Salaam jana.
Michuzi Media Group ikiongozwa Ahmad Michuzi mwanalibeneke wa Michuzijr Blog ( wa pili kulia) akiwa ameongozana na Mwanalibeneke wa Fullshwangwe Blog John Bukuku wakiwasili kwenye uzinduzi huo.
Aidha
alitoa rai kwa wanawake wengine hapa nchini ambao wanauwezo wa kuwa na
mitaji ya kuanzisha biashara wajiajiri na kutoa ajira kwa wengine pia
natoa wito kwa watanzania wengine waje katika duka la ZuRii kuja kutoa
sapoti kwa Jestina, alisema Magige.
Wakati
huohuo mmiliki wa duka hilo la ZuRii Jestina alisema kwamba yeye
ameona fursa za kuwekeza nyumbani hivyo ameamua kuzitumia ipasavyo.
“Natoa
wito kwa kwa wanadiaspora wenzangu ni kwamba wasiwe na tabia za kuja
likizo nyumbani nakuinjoi tu fedha zao tu bali wajitahidi kuja kuwekeza
kwani fursa zipo, kuanzisha duka hili ni ndoto yangu ya siku nyingi
hivyo haya ni matokeo ya njozi yangu namshukuru Mungu kwa kutimiza
ndoto hii”.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikata utepe
kuzindua rasmi duka la ZuRii House of Beauty linalomilikiwa na Mwana
Diaspora ambaye pia ni Blogger Jestina George Meru (anayeshuhudia tukio
hilo).
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiingia ndani ya duka hilo mara baada ya kulizindua.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa maelezo ya baadhi ya bidhaa
zake za urembo ambazo ni original kutoka nchini Uingereza na Marekani
kwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akiangalia
bidhaa za urembo wa nywele ndani ya dula la ZuRii House of Beauty
lililopo ndani ya jengo la Dar Free Market linalomilikiwa na Mwana
Diaspora Jestina George Meru.
Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akikagua moja ya bidhaa za nywele ndani ya duka hilo.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akitoa ushauri na maelezo kwa
baadhi ya wateja waliofika dukani kwake mara baada ya kuzinduliwa rasmi
jana jijini Dar.
Raia wa kigeni nao walivutiwa na bidhaa za duka la ZuRii House of Beauty.
Mwanalibeneke Khadija Khalili akiangalia baadhi ya bidhaa ndani ya duka ZuRii House of Beauty.
Wateja
wakiendelea kumiminika na kujichagulia bidhaa mbalimbali vikiwemo
vibanio vya nywele vya wakubwa kwa watoto ndani ya duka ZuRii House of
Beauty.
Mbunge
wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha, Mh. Catherine Magige akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) waliohudhuria uzinduzi huo
uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Mmiliki
wa duka la urembo la ZuRii House of Beauty na mwana Diaspora ambaye pia
ni mwanalibeneke Jestina George Meru akimpa mkono wa shukrani ya
kubariki uzinduzi duka hilo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Arusha,
Mh. Catherine Magige jana jijini Dar es Salaam.
- Mmiliki wa Duka la Zurii, Jestina George katika akizungumza na wanahabari katika uzinduzi wa duka hilo jana.
- Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.
- Jestina George kulia akizungumza na baadhi ya wanabloggers katika uzinduzi wa duka hilo jana.
- Baadhi ya wamiliki wa mitandao ya kijamii pamoja na waendeshaji wa mitandao hiyo wakiwa katika picha ya pamoja katika uzinduzi wa duka hilo.
: Wazalendo 25 Blog INAKUPONGEZA SANA Jestina George #Diasporah Blogger mmiliki wa Duka la Zurii house of Beauty kwa Kudhubutu na Kuweza. Mungu awe nawe
No comments:
Post a Comment