Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Kamillius Membe akizindua sherehe ya miaka 50 ya Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Dar es salaam, katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Albano, jijini Dar es salaam Jumapili, Januari 4, 2015, akishuhudiwa na Dk. Valentine Mokiwa, Askofu wa Dayosisi ya Dar es Salaam. |
Waziri Membe akizungumza katika sherehe hiyo |
Wachungaji wakimsikiliza Mheshimiwa Membe kwa makini wakati akiongea. |
Masista nao wakifuatilia |
Askofu Mokiwa akitoa mahubiri katika ibada ya uzinduzi wa sherehe ya miaka 50 ya Diyosisi ya Dar es Salaam. . |
Waziri Membe akisikiliza mahubiri yaliyokuwa yakitolewa na Askofu Valentino |
Waziri Membe akikaribishwa na Askofu Mokiwa kwaajili ya utoaji wa vitabu vya kuchangishia fedha kwa ajili ya miradi ya Dayosisi |
Waziri Membe aliaanza kumkabidhi kitabu cha Harambee Askofu Mokiwa |
Ibada ikiendelea. Picha na Reginald Philip |
======================================
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe, amelipongeza Kanisa la Anglikana Tanzania kwa kusimama kidete kupinga ndoa za jinsia moja, hata pale makanisa mengine ya Anglikana duniani yalipounga mkono suala hilo.
Akizindua
sherehe za Miaka Hamsini tangu kuanzishwa kwa Dayosisi ya Dar es Salaam
ya Kanisa hilo jana, Mhe. Membe alisema msimamo huo wa Kanisa na
Watanzania uliipa serikali nguvu kukataa shinikizom kutoka nchi za
Magharibi kwamba iidhinishe ushoga hapa nchini.
"Mlinitia
nguvu sana pale niliposimama kidete kuwaambia rafiki zetu wa nje kuwa
katika hilo la ndoa za jinsia moja, Tanzania tunaomba tukubaliane
kutokukubaliana," alisema Mhe. Waziri, wakati wa uzinduzi huo
uliofanyikia kwenye kanisa la Mtakatifu Albano, jijini Dar es Salaam.
Sherehe za Miaka 50 ya Dayosisi ya Dar es Salaam zitafikia kilele Julai,
mwaka huu.
Mhe.
Membe alisema serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Anglikana
na madhehebu mengine ya dini kuboresha maisha ya Watanzania. "Naomba
muendelee kushirikiana na serikali katika kutoa huduma kwa wananchi,"
aliwaambia waumini na waalikwa wengine waliohudhuria misa maalum ya
uzinduzi iliyoongozwa na Askofu Valentine Mokiwa.
Aliwataka
viongozi wa dini kuombea nchi umoja na amani, na kuhimiza waumini wao
kushiriki kikamilifu katika matukio mawili muhimu yanayolikabili taifa
mwaka huu -- Kura ya maoni ya Katiba inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa
Rais na Wabunge.
Uchaguzi
wa Rais ni muhimu kwa sababu "Rais wa Awamu ya Tano atategemewa
kuendeleza mema ya Awamu ya Nne na awamu zilizopita, na kutoa majawabu
kwa changamoto za sasa na zijazo na kutusogeza karibu zaidi na Tanzania
njema tunayoitamani, Tanzania yenye neema tele. Hatuko mbali na nchi
yetu hiyo ya ahadi," alisema.
Mhe.
Membe alishambulia rushwa na Ufisadi kuwa ndivyo vinavyodidimiza nchi
na kuongeza umasikini kwa wananchi licha ya Tanzania kuwa na rasilimali
lukuki.
"Tuchague viongozi waadilifu, wazalendo, wachapa kazi, wasio na uchu wa madaraka kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi na marafiki zao," alisema.
"Tuchague viongozi waadilifu, wazalendo, wachapa kazi, wasio na uchu wa madaraka kwa ajili ya kujinufaisha wao binafsi na marafiki zao," alisema.
Alitaka
vijana waandaliwe vyema kushiriki ujenzi na ulinzi wa taifa kwani ndio
warithi. "Tukiwaandaa vyema,mustakabali wa taifa letu na watu wake
utakuwa kwenye mikono salama. Tukishindwa leo, tutalia na kusaga meno
kesho," alionya.
No comments:
Post a Comment