Meneja
Mauzo wa StarTimes Tanzania, David Kisaka (kushoto) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa bei mpya ya
king’amuzi kitakakochouzwa kwa shilingi 4000 sambamba na kifurushi kipya
cha NYOTA cha malipo ya 4000 kwa mwezi, kulia pamoja naye ni Mkurugenzi
wa Masoko na Mauzo, Jacky Yu. Bei hiyo mpya ya king’amuzi na kifurushi
itamfanya mteja afurahie chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za kimataifa
na 7 za nyumbani kwa muda wa miezi saba na nusu.
Baadhi
ya wateja waliokuwepo kwenye uzinduzi wa bei mpya ya king’amuzi
kitakakochouzwa kwa shilingi 4000 sambamba na kifurushi kipya cha NYOTA
cha malipo ya 4000 kwa mwezi. Bei hiyo mpya ya king’amuzi na kifurushi
itamfanya mteja afurahie chaneli zisizopungua 16 ikiwa 9 ni za kimataifa
na 7 za nyumbani kwa muda wa miezi saba na nusu. Uzinduzi huo
ulifanyika katika duka la kampuni hiyo lililopo ofisi za TBC1,
Mikocheni-Bamaga jijini Dar es Salaam.
Kuhakikisha
kila mtanzania anapata huduma bora na nafuu za matangazo ya dijitali,
StarTimes imekuja na kifurushi kipya na bei mpya ya king’amuzi kwa
shilingi 4000/- tu gharama ambayo ni ya chini kabisa kutowahi kutokea
nchini.
Akizungumzia
juu ya huduma hii mpya Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa kampuni ya Star
Media Tanzania ambao ni wauzaji wa ving’amuzi vya StarTimes nchini, Bw.
Jacky Yu amebainisha kuwa uzinduzi huu ni sehemu ya kutimiza ahadi kwa
watanzania kwamba watakuwa wakitoa huduma bora na kwa bei nafuu ambayo
kila mtu ataweza kuimudu.
“Leo
tunayo furaha kubwa kabisa kuwatangazia umma wa watanzania kwamba
StarTimes imeshusha bei ya king’amuzi chake mpaka kufikia shilingi 4000
na kuzindua kifurushi kipya na cha bei ya chini kinachokwenda kwa jina
la NYOTA ambacho kitapatikana kwa malipo ya shilingi 4000 kila mwezi.”
“Kifurushi
hiki kipya cha NYOTA kina jumla ya chaneli zisizopungua 16, saba ni za
nyumbani na 9 ni za kimataifa ambazo ni Star Swahili, Bollywood Swahili,
E-Star, Star Music, Kungfu 1, Child Smile, TBN, TV Imani na CCTV News.
Ili mteja aweze kuunganishwa na kifurushi hiki itabidi aambatanishe na
malipo ya awali ya shilingi 30,000 na kuweza kufaidi kwa muda wa miezi
saba na nusu.” Alifafanua zaidi Bw. Yu
Aliendelea
kwa kusema kuwa, baada ya muda wa ofa iliyotolewa kwa wateja wa
kifurushi kipya cha NYOTA kuisha, mteja ataamua kama anaendelea na
kifurushi hiki cha kulipia shilingi 4000 kila mwezi au kutazama vingine
vya kawaida. Ili mteja kurudishwa katika vifurushi vya kawaida ambavyo
vitamruhusu kutazama chaneli za bure za nyumbani na kulipia vifurushi
vilivyopo basi itambidi afuate njia ya kawaida ya kujiunga ambayo ni
rahisi kwa kupiga *150*63# na kufuata maelekezo au atembelee ofisi zetu
na za mawakala.
“Madhumuni
makubwa ya bei hii mpya ya king’amuzi na kifurushi cha NYOTA ni kumtaka
kila mtanzania hata Yule wa kipato cha chini aweze kupata matangazo ya
dijitali. Tuna imani kubwa kwamba kifurushi hiki kipya kitakidhi
mahitaji ya wateja wetu wote ambao wanapenda huduma zetu lakini
hushindwa kulipia gharama za vifurushi vilivyopo.” Alisema Bw. Yu na
kumalizia, “Siku zote StarTimes tutaendelea na dhamira yetu ya kutoa
huduma za uhakika na kwa bei nafuu ili kumfikia kila mteja. Tunaimani
matangazo ya dijitali ni fursa ambayo kila mtanzania lazima anufaike
nayo.”
Naye
kwa upande wake Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Bw. David Kisaka
aliongezea kwa kusema, “kifurushi hiki kipya kimeongezewa katika
vifurushi vyetu vilivyopo, hivyo basi kuanzia leo hii tutakuwa na jumla
ya vifurushi vinne ambavyo ni NYOTA, Mambo, Uhuru na Kili.
Tulichoongezea ni unafuu na kuwajali wateja wetu kwani tunatofautiana
kwa hali za kiuchumi na tunafahamu kwamba watanzania wengi ambao ni
wateja wanavipato vya kawaida. Tunaamini kwa kifurushi hiki kipya cha
NYOTA sasa tutawafikia watanzania wote na kuwawezesha kufurahia
matangazo ya dijitali.”
“Ningependa
kutoa wito kwa wateja wetu kutembelea maduka yetu na ya mawakala wetu
popote yalipo ili kuweza kuhudumiwa au kupiga namba ya huduma ya wateja
ambayo ni 0764 700 800 ili kupata maelezo na ufafanuzi zaidi. Na pia
ningependa kuwatoa hofu huduma hii ni endelevu kwani ni mwanzo tu wa
maboresho ya huduma zetu kwani kuna mabo mazuri lukuki yapo njiani
yanakuja. Na kwa wale wasio wateja wetu basi huu ndio muda muafaka kwa
wao kuunganishwa na huduma zetu, wameshapitwa na mengi lakini hili si la
kuliacha lipite hivi hivi.” Alihitimisha Bw. Kisaka
No comments:
Post a Comment