Biashara na Mazingira : Mh. Ummy Mwalimu ziarani jijini Arusha - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 22 January 2015

Biashara na Mazingira : Mh. Ummy Mwalimu ziarani jijini Arusha


Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu (katikati) akiwa katika mazungumzo na baadhi ya watendani wa viwanda jijini Arusha wakati akiwa kwenye ziara ya kikazi ya siku moja katika baadhi ya viwanda vya Arusha lengo likiwa ni kufuatilia utekelezaji wa maagizo ya Serikali kuhusu viwanda kutotumia magogo kama nishati ya uzalishaji viwandani
Moja ya boiler inayotumia makaa ya mawe katika Kiwanda cha Sunflag. Awali Kiwanda hicho kilikuwa kinatumia nishati ya Magogo katika shughuli za uzalishaji kiwandani hapo. Serikali imepiga marufuku matumizi ya magogo ili kuhifadhi mazingira.
Shehena ya magogo iliyobaki katika Kiwanda cha Sunflag. Kiwanda hicho kwa sasa kimebadilisha matumizi ya nishati ya uzalishaji kutoka kwenye magogo na kutumia makaa ya mawe.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Bw. Binesh Haria Afisa Mwendeshaji wa Kiwanda cha A to Z cha Jijini Arusha. Naibu Waziri alikuwa na ziara ya ukaguzi wa masuala ya Mazingira kiwandani hapo.
Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Ummy Mwalimu akiongea na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha Bw. Fidelis Lumato mara baada ya kutembelea kiwanda cha A –Z cha Jijini hapo kukagua masuala ya Mazingira.

No comments:

Post a Comment