Mkuu
wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu (kushoto) akimuongoza Kiongozi wa
Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina Makilagi
aliyeambatana na wajumbe wengine wa kamati hiyo baada ya kuwasili ofisi
za Mradi wa Maji Kibiti ulioko wilayani humo mkoani Pwani kabla ya
kuukagua.Ukaguzi wa mradi huo ni sehemu ya ziara ya ukaguzi wa miradi ya
maji katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara inayofanywa na wajumbe wa
Kamati hiyo.
Meneja
wa Mradi wa Maji Kibiti Mhandisi Juma Ndaro akitoa ufafanuzi kwa kamati
ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, juu ya mradi huo wakati kamati
ilioptembelea kukagua mraddi huo.
Kiongozi
wa Wajumbe wa Kamati Amina Makilagi akipanda ngazi za tanki la maji la
mradi wa maji wa Kibiti wakati akikagua mradi huo, huku Mkuu wa Wilaya
ya Rufiji Nurdin Babu na watendaji wengine wakishuhudia.
Mhandisi
wa Maji mkoa wa Pwani Mhandisi Alphonce (kulia), akiwaeleza jambo
baadhi ya wajumbe wa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji wakiwa
juu ya tanki la maji la mradi wa Kibiti.Kutoka kushoto ni Amina Makilagi
(Mb) Kiongozi wa wajumbe, Meneja Mradi wa Ikwiriri Ladislaus Komba,
Asaa Hamad (Mb),Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu, Abdallah Haji Ali
(Mb).
Mwenyekiti
wa Mtaa wa Mtawanya Kati Mwanaisha Mohamed akieleza hoja yake mbele ya
wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji walipotembelea
mradi wa maji Kibiti.
Meneja
wa Mradi wa Maji Ikwiriri Ladislaus Komba (aliyeshika jalada) akitoa
ufafanuzi wa mradi huo mbele ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo,
Mifugo na Maji na watendaji wa wilaya ya Rufiji na wawakilishi wa
Ikwiriri, baada ya kuwasili kwenye tanki la mradi huo.
Kiongozi
wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Amina
Makilagi akinywa maji yaliyotoka kwenye kisima cha mradi wa maji
Ikwiriri wilayani Rufuji mkoani Pwani, kwenye ziara ya kamati hiyo
kukagua miradi ya maji katika mikoa ya Pwani, Lindi na Mtwara.
Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji, Wawakilishi wa wananchi
wa Ikwiriri na wataalamu wa Wizara ya Maji, wakiwa kwenye eneo la mtambo
wa kusukumia maji wa mradi wa maji wa Ikwiriri, kukamilisha ziara ya
kukagua miradi ya maji wa Ikwiriri.
Picha zote na Hussein Makame, MAELEZO
No comments:
Post a Comment