Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(katikati) akikata utepe kufungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na
Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo
(kushoto) Waziri wa Afya Rashid Seif Suleiman na Prof,Dk. Mahmoud Quresh
Mwakili wa taasisi ya ND kutoka Spein sherehe hizo ikiwa ni sehemu
ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Dk.Mohamed Ali Haji (ustadh)
wa sehemu ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit)
katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja wakati Rais alipowatembelea wagonjwa
mbali mbali waliokwisha fanyiwa matibu na Kituo hicho baada ya
kulifungua jengo hilo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
na Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif wakimuangalia Mtoto Iman
Haroun Mbarouk Miezi minne (4) wa Kijichi akiwa na Mama yake Asha
Mohamed Said akiwa tayari amesha fanyiwa upasuaji wa kichwa katika kituo
cha (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja baada ya
kulifungua jengo hilo leo ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
(wa pilikushoto) na Makamo wa Kwanza wa Reais maalim Seif Sharif Hamad
wakipata maelezo kutoka kwa Prof,Dk. Mahmoud Quresh Mwakili wa taasisi
ya ND kutoka Spein wakati alipotembelea mashine za upasuaji baada ya
kulifungua jengo jipya ya upasuaji wa Ubongo na Uti wa Mgongo
(Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya Mnanzi Mmoja leo (kulia)
Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali Dk.Jamala Adam Taibu pia sherehe hizo
ikiwa ni sehemu ya Maadhimisho ya miaka 51 ya Mapinduzi Matukufu ya
Zanzibar.
Wanafunzi
wa Chuo cha Sayansi ya Afya wakiwa mbele ya jengo la jipya ya upasuaji
wa Ubongo na Uti wa Mgongo (Neurosurgical Unit) katika Hospitali ya
Mnanzi Mmoja baada ya kufunguliwa rasmi leo na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein likiwa la horofa
mbili na uwezo wa vitanda 30 pamoja na vyumba (2)viwili vya
upasuaji.Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment