Taswira Muhimu : Rais Jakaya Kikwete Akutana na Diamond Platnumz na Kumpongeza Juu ya Ushindi Wake wa Tuzo Tano za Muziki za Kimataifa Mwaka Huu - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


29 Dec 2014

Taswira Muhimu : Rais Jakaya Kikwete Akutana na Diamond Platnumz na Kumpongeza Juu ya Ushindi Wake wa Tuzo Tano za Muziki za Kimataifa Mwaka Huu



 Rais Kikwete akiwa na msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kumkaribisha na kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014. Kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko, na kushoto ni katibu wa Bodi ya filamu Tanzania Bi. Joyce Fissoo.
 Tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda Naseeb Abdul “Diamond” mwaka huu 2014.
 Rais Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Hermas Mwansoko.
 Rais Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond” na kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014.
 Rais Kikwete akipokea CD mpya ya msanii Naseeb Abdul “Diamond” baada ya kuoneshwa tuzo tano za muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014.
 Rais Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Naseeb Abdul “Diamond” juu ya ushindi wake wa tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014.
Rais Kikwete akiongea na msanii Naseeb Abdul “Diamond” alipomkaribisha Ikulu kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23, 2014.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad