Miss
Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate
Mwegelo, akimpa zawadi ya ndala mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo
cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea
kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni
mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti.
Miss
Tanzania namba mbili 2006, Mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate
Mwegelo, akicheza na mmoja wa watoto wanaolelewa katika Kituo cha Yatima
cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea kuwapa
zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni mchele,
unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti.
Miss
Tanzania namba mbili 2006, mwanamitindo na mcheza filamu, Jokate
Mwegelo, akiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika Kituo
cha Yatima cha Extrem cha Tandale kwa Bi Mtumwa Jumanne, alipotembelea
kuwapa zawadi ya Sikukuu ya Krismas na Mwaka Mpya. Zawadi alizotoa ni
mchele, unga wa sembe, sabuni na ndala zenye nembo za Kidoti. Picha na
Jumanne Juma.
--
MISS
Tanzania namba mbili 2006, mbunifu mavazi na muigizaji wa filamu za
kibongo, Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, leo ametoa msaada wa vitu mbalimbali
katika Kituo cha Kulea Yatima cha Extrem kilichopo Tandare kwa Bi
Mtumwa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mrembo
huyo ambaye pia ni mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti inayojihusisha na
masuala ya urembo, alitoa msaada huo kama zawadi yake ya Sikukuu ya
Krismas na Mwaka Mpya kwa watoto hao kama sehemu ya kuwafariji ili nao
kujiona wako sawa na wengineo wanaioshi nawazazi wao.
Akizungumza
mara baada ya kukabidhi msaada huo, Jokate alisema kuwa ameguswa na
kituo hicho ambacho huwa hakikumbukwi na wahisani kutokana na mazingira
ya eneo hilo.
“Nimefika
hapa kutoa msaada kama sehemu ya kuonyesha ninavyoguswa na jamii ya
watoto kama hawa, lakini pia nikiwa na lengo la kuwafariji ili nao
kujiona ni sehemu ya jamii ya Watanzania,” alisema.
Kidoti
alitumia fursa hiyo kutoa wito kwa watu wenye uwezo, kampuni na taasisi
mbalimbali kuona umuhimu wa kusaidia makundi hayo maalumu katika jamii
kwani nao wana haki ya kuishi na kufurahia maisha kama wengine.
Msaada
aliokabidhi kwa ushirikiano na kampuni ya Raibow Shell, ni mchele, unga
wa sembe, sabuni, jozi za viatu vyenye nembo za Kidoti.
Akizungumza
baada ya kupokea msaada huo, mlezi wa watoto hao, Mwamvua Jumanne,
alitoa pongezi kwa Kidoti na kuwasihi wengine kuiga mfano wa mrembo huyo
kusaidia makundi maalum.
Akielezea
changamoto zilizopo katika kituo hicho, Mwamvua alisema ni kukosa uwezo
wa kifedha kuwalipia ada watoto wanaosoma elimu ya msingi na sekondari,
gharama za matibabu pamoja na kukosa watu wa kuwatembelea ili
kuwafariji.
No comments:
Post a Comment