Waziri
Mkuu, Mh. Mizengo Pinda na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison Mwakyembe
wakikagua moja ya mabehewa mapya ya TRL yaliyonunuliwa kwa fedha ya
serikali wakati alipokwenda kwenye Bandari ya Jijini Dar es salaam Desemba 8, 2014 kupokea mabehewa hayo.
Waziri
Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiongozwa na Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Harrison
Mwakyembe (kulia kwake) na Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba
(kulia) kukagua baadhi ya mabehewa mapya ya Shirika la Reli nchini (TRL)
yaliyonunuliwa na kwa fedha za serikali wakati alipokwenda kwenye
bandari ya jijini Dar es salaam Desemba 8,2014.
Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiangalia jiko ambalo liko ndani ya behewa la
daraja la pili kwenye moja ya mabehewa 22 yaliwasili nchini mwisho wa
wiki, katika bandari ya jijini Dar es Salaam,Desemba 8,2014.
Waziri
Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akishuka kwenye moja ya mabehewa 22
yakiyowasili nchini mwisho wa wiki, leo mchana katika bandari ya Dar es
Salaam.Mh. Pinda alifika Bandarini hapo kukagua mabehewa hayo. Waziri
Mkuu amempongeza Waziri wa Uchukuzi pamoja na watendaji wake kwa kazi
nzuri wanayoifanya katika Kuimarisha usafiri wa Reli nchini. Utekelezaji
wa mradi huu ni mojawapo wa Miradi inayotekelezwa chini ya mpango wa
matokeo makubwa sasa(BRN).
Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akimsikiliza Naibu Waziri wake, Dkt. Charles Tizeba leo mchana katika bandari ya Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment