Rais
Wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Mh Jamal Malinzi
akizungumza na wanahabari leo katika ofisi za TFF kuhusu kampuni ya
Proin Promotions ltd kudhamini Mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake
yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa, mashindano hayo yanatarajiwa
kuanza tarehe 28 Disemba kwa kushirikisha timu kutoka Mikoa yote ya
Tanzania. Mashindano hayo yatazinduliwa Mkoani Mwanza kwa kuzikutanisha
timu za Mwanza na Mara. Kushoto kwa rais wa TFF ni Rose Kissiwa ambae ni
mwakilishi wa Chama cha Mpira wa wanawake Tanzania.Na Kulia ni
Mkurugenzi wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza ambao ndio wadhamini
wakuu wa Kombe la Wanawake Tanzania
Rais
wa TFF akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari
(Hawapo pichani) kuhusiana na Kombe la Wanawake Taifa ambapo ni
mashindano ya mpira wa miguu kwa wanawake yaliyodhaminiwa na Kampuni ya
Proin Promotions Ltd.
Mkurugenzi
wa Makampuni ya Proin , Johnson Lukaza akizungumzia jinsi kampuni ya
Proin Promotions Ltd ilivyoona umuhimu wa kuchangia katika kuinua soka
la wanawake nchini na kuamua kudhamini Shindano hilo lijulikanalo kama
Kombe la Wanawake Taifa ambalo litaanza rasmi tarehe 28 kwa mechi ya
uzinduzi kati ya Mwanza na Mara huko Mkoani Mwanza
Meneja
Biashara wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania (TFF) Peter Simon
akizungumzia juu ya ratiba ya mashindano hayo yajulikanayo kama Kombe la
Wanawake Taifa ambapo timu za wanawake kutoka mikoa yote ya Tanzania
zitashiriki katika mashindano hayo yaliyodhaminiwa na Kampuni ya
Usambazaji na utenegenezaji wa Filamu za Kitanzania ijulikanayo Kama
Proin Promotions Ltd
Bi
Rose Kissiwa, Mwakilishi wa Chama cha Mpira wa Wanawake Tanzania
akizungumzia juu ya udhamini uliotolewa na kampuni ya Proin Promotions
Ltd katika kufanikisha Mashindano ya Mpira wa miguu kwa Wanawake
yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa ambapo uzinduzi wa Mashindano
hayo yatafanyika Jijini Mwanza kwa kuzikutanisha TImu za Mwanza na
Mara.Picha zote na Josephat Lukaza wa http://www.josephatlukaza.com
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Nchini Tanzania (TFF) leo imemtambulisha rasmi
Kampuni ya Proin Promotions Ltd kuwa mdhamini mkuu wa Mashindano ya
Mpira wa Miguu kwa wanawake yajulikanayo kama Kombe la Wanawake Taifa
ambapo mashindano hayo yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 28
Disemba 2014 katika Uwanja wa CCM kirumba jijini Mwanza kwa
kuzikutanisha timu za Mwanza na Mara.
Akizungumzia
Udhamini huo uliotolewa na Kampuni ya Proin Promotions Ltd, Rais wa TFF
jamal Malinzi amesema kuwa Anawashukuru kwanza Proin Promotions Ltd kwa
kuona umuhimu pia wa kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa wanawake hapa
nchini kwa kudhamini mashindano ya Kombe la Wanawake Taifa ambapo
katika mashindano hayo timu kutoka mikoa yote ya Tanzania zitashiriki na
hatimaye kuja kupata Mshindi. Mbali na Mashindano hayo Mechi zote za
Mashindano hayo zitarekodiwa na kuweza kurushwa katika vituo mbalimbali
vya habari ambapo watanzania watapata nafasi ya kuwapigia kura wachezaji
bora katika kila nafasi na kuwawezesha kushinda.
Akizungumzia
Swala hilo Mkurugenzi Wa Makampuni ya Proin Promotions Ltd, Bw Johnson
Lukaza amesema kuwa mpaka sasa Mazungumzo bado yanaendelea na wamiliki
wa Vituo vya Televisheni ili kuona uwezekano wa wao kurusha Mashindano
hayo na kuwawezesha watanzania kuwapigia kura wachezaji. ameongezea kwa
kusema kuwa Mara tu mazungumzo hayo yakimalizika na kuweza kupata nafasi
kutoka kituo chochote cha Televisheni ambacho kitakubali kurusha
mashindano hayo basi umma wa watanzania watatangaziwa.
Proin
Promotions Ltd ambao ndio wadhamini wakuu wa Mashindano hayo ya Kombe
la Wanawake Taifa inatoa nafasi pia kwa makampuni mengine katika kujitoa
na kuungana nao ili kuweza kukuza vipaji vya mpira wa miguu kwa
wanawake lengo likiwa ni kuboresha Timu ya Taifa ya wanawake Tanzania.
No comments:
Post a Comment