Mwenyekiti
wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim
Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa
wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya
kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam . Majadiliano
hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa
hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania
(Bloggers). Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo ya muda kutoka Zanzibar,
Othman Maulid.
Katibu
Msaidizi wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha
(kushoto),akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo wakati wa mapitio ya
rasimu hiyo. Kulia ni Mjumbe wa Kamati, Henry Mdimu.
Mwenyekiti
wa Muda wa Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers), Joachim
Mushi (wa pili kushoto), akizungumza wakati akifungua majadiliano kwa
wajumbe wa kamati ya muda ya wamiliki wa mitandao ya jamii Tanzania ya
kujadili rasimu ya Katiba ya umoja huo Dar es Salaam . Majadiliano
hayo yameanza jana kujadili rasimu ya katiba kabla ya kuipitisha kwa
hatua za usajili wa Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania
(Bloggers). Kutoka kushoto ni Mjumbe, Othman Maulid, Katibu Msaidizi wa
Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania , Shamim Mwasha, Henry Mdimu
(Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe) na William Malecela (Mjumbe).
Wajumbe wa kamati hiyo wakiwa katika picha ya pamoja baada ya mkutano wao uliofanyika katika Mgahawa wa MOG Longue, jijini Dar es Salaam asubuhi.
***********
Na Dotto Mwaibale,
WAJUMBE
wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania (Bloggers)
wameanza vikao vyao kujadili rasimu ya katiba ya umoja huo kabla ya
kufanya usajili wa chama chao kitakacho waunganisha wamiliki na
waendeshaji wa mitandao hiyo Tanzania.
Akizungumza
leo katika vikao hivyo vinavyofanyika jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti
wa Muda wa Kamati ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania, Joachim
Mushi amesema wajumbe waliokutana ni wawakilishi wa wamiliki wa mitandao
hiyo kutoka makundi mbalimbali ya waendeshaji hao wa mitandao ya jamii
nchini.
Alisema
pamoja na mambo mengine wajumbe hao wanatarajia kufanya majadiliano
baada ya kuipitia rasimu ya Katiba ikiwa ni kuelekea mchakato wa kupata
Katiba ya Chama cha Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania. Alisema
masuala mengine ambayo yataongoza mjadala huo ni pamoja na kuangalia
muundo wa chama, uendeshaji wake, maadili ya chama kwa wanachama katika
utekelezaji kazi zao.
"Kikao
hiki kinashirikisha wajumbe wa kamati ambao ni wawakilishi wa makundi
mbalimbali ya wamiliki na waendeshaji wa mitandao ya jamii Tanzania na
kazi kubwa ambayo wataifanya leo kwa pamoja ni kupitia rasimu ya uumoja
wetu. Wajumbe wote walikabidhiwa rasimu hii wiki mbili zilizopita
kuipitia wenyewe kabla ya kukutaka katika majadiliano ya leo," alisema
Mwenyekiti wa Muda, Mushi.
Aidha
aliishukuru Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa mchango wake wa
dhati wa kuwaunga mkono Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania hasa
katika kipindi hiki cha mchakato kuelekea uundwaji wa chama chao.
Miongoni
mwa wajumbe wa kamati hiyo ya muda waliokutana ni pamoja Shamim Mwasha
(Katibu Msaidizi) Khadija Kalili (Katibu), Joachim Mushi (Mwenyekiti),
Henry Mdimu (Mjumbe), Mariam Ndabaganga (Mjumbe), William Malecela
(Mjumbe), Othman Maulid (Mjumbe-Zanzibar) na Francis Godwin (Makamu
Mwenyekiti - Iringa).
Mkutano
wa mafunzo wa idadi kubwa ya wawakilishi wa wamiliki wa mitandao ya
kijamii nchini (Bloggers) uliofanyika Novemba 11, 2014 jijini Dar es
Salaam ulioitishwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania uliibua uundwaji
wa Kamati ya Muda ya Wamiliki wa Mitandao ya Jamii Tanzania chini,
ambapo kamati hiyo ilipewa jukumu la kupitia rasimu kabla ya
kushughulikia usajili wa chama cha jumuia hiyo.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com)
No comments:
Post a Comment