Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete kuzungumza na Wazee wa mkoa wa Dar
es Salaam kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alimpa taarifa
Mheshimiwa Rais juu ya mafanikio ya ujenzi wa maabara katika Shule za
Sekondari mjini Dar es Salaam pamoja na matokeo ya uchaguzi wa Serikali
za mitaa.(Picha zote na Adam Mzee)
Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia Wazee wa
mkoa wa Dar es Salaam ambao waliitika wito wa kumsikiliza wakati wa
kulihutubia Taifa kupitia Wazee kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini
Dar es Salaam.( Picha na Adam Mzee
Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akisoma hotuba yake kwa Wazee wa mkoa wa Dar es Salaam kwenye
ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam. ( Picha na Adam Mzee)
Baadhi ya Wanasiasa wakongwe waliohudhuria.
Kila wilaya ya mkoa wa Dar es salaam iliandaliwa sehemu maalum ya kukaa.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Taifa kupitia Wazee wa mkoa wa Dar es
Salaam katika ukumbi wa Diamond Jubilee ambapo alizungumzia uchaguzi na
kutaka polisi kufanya kazi yao katika kuhakikisha uchaguzi ujao uchaguzi
hauvurugwi na pia alifafanua mambo mbali mbali yaliyokuwa
yakizungumziwa kuhusu akaunti ya ESCROW na kumwajibisha Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka.
Ukumbi
wa Diamond Jubilee ukiwa umefurika Wazee waliokuja kumsikiliza
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete.
Ukumbi ulifurika kila kona.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati wa ufafanuzi wa masula
kadhaa yaliyoleta mkanganyiko kwenye sakata la Escrow Akaunti.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Jakaya mrisho Kikwete akipanga
makaratasi yenye hotuba yake wakati wa kuhutubia Wazee wa mkoa wa Dar es
Salaam.
Wananchi wakishangilia
baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhitimisha hotuba yake
kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar Es Salaam.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipongezwa na mbunge wa Kionondoni Mhe.
Iddi Azzan muda mfupi baadaya baada ya kulihutubia taifa kwa kupitia
wazee wa Dar es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam
Mwanasiasa
Mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akimpongeza Rais Dkt.Jakaya Mrisho
Kikwete muda mfupi baada ya kulihutubia taifa kwa kupitia wazee wa Dar
es Salaam leo katika ukumbi wa Diamond jijini Dar es Salaam
No comments:
Post a Comment