Wafanyakazi
wa kituo cha redio 5 Arusha wakikabidhi misaada mbalimbali katika
kampeni ya “USHINDI”inayoendeshwa na kituo hicho,misaada hiyo ilitolewa
na wahisani mbalimbali kwaajili ya watoto wanaoishi katika vituo vya
watoto yatima Mkoani Arusha,katika Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky
Mwakoyo kushoto ni Sarah Keiya wakiwakabidhi watoto wa kituo cha
kiwohede ndoo ya mafuta ya kupikia kwaajili ya sikukuya Krismass na
mwaka mpya jijini hapa jana katika hotel ya world Garden
Wafanyakazi
wa kituo cha redio 5 wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wa kituo
cha kiwohede na huruma katika hotel ya world Garden iliyopo moshono
jijini Arusha
Mkuu wa vipindi wa kituo hicho Mathew Philip akikabidhi moja ya msaada kwa shcha watoto huruma
Watoto wanaoishi katika vituo vya watoto yatima wakishindana kucheza muziki
Grace Joseph(12)wa kituo cha kiwohed akionyesha ujuzi wake wa kucheza katika shindano
Mtoto anayeishi katika mazingira magumu akiwa jukwaani akiimba wimbo wa “NISEME”wimbo wa moto band
Mashindano yakiwa yanaendelea
Wafanyakazi wa Redio 5 wakiwa mzigoni
Meneja
ubunifu wa Redio 5 Vicky Mwakoyo akiwa anamkabidhi zawadi ya kikombe
mshindi namba moja katika shindano la kucheza muziki
Wafanyakazi wa redio5 wakiwa wanaanda sausage kwaajili ya watoto yatima
Muonekano wa watoto wakiwa katika eneo la kuchezea michezo mbalimbali
Meneja ubunifu wa Redio 5 Bi.Vicky Mwakoyo akiwa Meneja masoko wa Redio 5 Bi.Sarah Keiya
Mtangazaji
wa kituo hicho Akiba Kilango ambaye alikuwa MC wa shughuli hiyo akiwa
anaongea na watoto jukwaani kabla ya mashindano ya kucheza kuanza
Wafanyakazi wa kituo hicho wakiwa katika maandalizi ya kuwaandalia watoto mapochopocho
Kulia
ni mtoto Sharon Nelson akiwa anakabidhi msaada alioleta katika kampeni
ya ushindi amewataka watoto wengine kujitolea kusaidia wasionacho
Mtoto mwenye ulemavu wa ngozi akiwa anafatilia tamasha hilo
Kampuni Tan Communication Media
inayo miliki kituo cha Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha
imeeanda tamasha kwa watoto yatima wanaoishi katika vituo lenye jina
“Kampeni ya USHINDI”linalowashirikisha wadau mbalimbali wa mkoa wa
Arusha
Mkurugenzi wa kituo hicho Robert
Francis anachukua jukumu la kuwasihi jamii kwa ujumla kuwa na tabia ya
kuwakumbuka mayatima hasa kipindi hichi cha sikukuu ili nao wasijione
kutengwa
Meneja ubunifu wa Redio 5 Vicky
Mwakoyo alisema kuwa kila mtoto anastahili kuwa na furaha na baadhi yao
ni wale wenye uwezo mdogo ni vyema kuwakumbuka na tusiwatenge na
tukifanya hivi watajiskia vizuri
Meneja masoko wa Redio 5 Sarah Keiya
ametoa shukrani kwa wadau wote walioshirikiana na kituo hicho kwa
kuwezesha kampeni hiyo kufanikiwa,wadau wakubwa walioshiriki ni Redio
5,Pepsi,Fifis bakery,Arusha meat,Skytel,Monaban,Vibration duo,Brundful
company,World garden. Picha na Pamela Molel wa Jamii Blog
No comments:
Post a Comment