Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda akila kiapo
mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika hafla iliyofanyika ikulu
jijini Dar es Salaam Jumatatu Desemba 8, 2014 na kuhudhuriwa na Waziri
Mkuu Mizengo Pinda na viongozi wengine waandamizi wa serikali.Katikati
wapili kushoto anayeshuhudia ni Katibu mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
na watatu kushoto ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gervas Mdemu
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa miongozo ya kazi(Standing
Orders) Mkuu mpya wa Mkoa wa Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa
hafla ya kuapa iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam
Jumatatu Desemba 8, 2014
asubuhi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Mkuu mpya wa mkoa wa
Arusha Mhe.Daudi Felix Ntibenda wakati wa hafla wa kuapa iliyofanyika
ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amembeba mtoto Gracious Mathayo
Ntebo mjukuu wa wa mkuu mpya wa Arusha Mhe. Daudi Felix Ntibenda wakati
wa hafla ya kumuapisha mkuu huyo wa mkoa iliyofanyika ikulu jijini Dar
es Salaam
Jumatatu Desemba 8, 2014
. Picha na Freddy Maro
No comments:
Post a Comment