Maisha Yetu : Dk. Reginald Mengi Azindua TASWE SACCOS Jijini Dar - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 11 December 2014

demo-image

Maisha Yetu : Dk. Reginald Mengi Azindua TASWE SACCOS Jijini Dar


IMG_3785
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) uliofanyika katika ukumbi wa St. Peter's jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs (TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde na  Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal.  Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.
IMG_3834
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akishirikiana na Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal.IMG_3822
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikabidhiwa zawadi kwa mchango wake anaoutoa katika jamii.
IMG_3706
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akiongea machache.
IMG_3652
Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii ili kupambana na changamoto za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na kuwajengea watanzania tabia ya kuweka akiba.
IMG_3631
IMG_3577
IMG_3587

Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akikagua miradi mbali mbali inayoendeshwa na akina mama wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) wakati wa uzinduzi uliofanyika katika ukumbi wa St. Peter's jijini Dar es Salaam.
IMG_3608
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi akionyeshwa jiko la kisasa linalopunguza matumizi. Pembeni kwake ni Balozi Mdogo wa India, Baluinder Humpal katikati wakiongozwa na mwenyeji wao Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde.
IMG_3630
Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Media, Dk. Reginald Mengi Disemba 10, 2014 amezindua Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss) itakayowawezesha watanzania na wanachama kuweka akiba, kukopa na kununua hisa kwaajili ya kupata mitaji ya kuboresha shughuli zao za kijamii na kiuchumi.
IMG_3849
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tanzania Saccos For Women Entrepreneurs ( TASWE - Saccoss), mama Anna Matinde alisema "Tumeanzisha Saccos hii ili kupambana na changamoto za upataji wa mikopo kwa riba kubwa na kuwajengea watanzania tabia ya kuweka akiba. Mpaka sasa tuna wanachama zaidi ya 200 hapa Dar es Salaam na tumejipanga kutanua wigo na kufungua matawi zaidi Kanda ya Kaskazini, mikoa ya Dodoma, Mtwara, Lindi, Mwanza hadi ifikapo mwezi wa tatu mwakani.
Lakini pia ipo miradi tuliyonayo yenye lengo la kuinua na kukuza chama hiki cha saccoss na kunufaisha wanachama wake. Ofisi zetu ziko Oysterbay, Dar es Salaam hivyo nawakaribisha wanachama wapya kujiunga
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa email annamatinde@gmail.com au 0754692994.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *