Matukio : Mhe. Anne Makinda Ashiriki Misa Maalum ya Kumuombea Aliyekuwa Rais wa Zambia Marehemu Michael Sata, Lusaka Zambia - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Tuesday, 11 November 2014

Matukio : Mhe. Anne Makinda Ashiriki Misa Maalum ya Kumuombea Aliyekuwa Rais wa Zambia Marehemu Michael Sata, Lusaka Zambia


Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake.
Aliyekuwa Rais wa Serikali ya Awamu wa Zambia Mhe. Lupia Banda akimpokea Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda alipowasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kushiriki Misa Maalum ya Kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Chilufya Sata kabla ya maziko yake kufanyika leo.
Rais wa Bunge la SADC na Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda akishiriki Misa Maalum ya kumwombea aliyekuwa Rais wa Zambia Mhe. Michael Sata katika viwanja vya Bunge la Zambia leo. Mwili wa Marehemu Sata unatarajia kuzikwa leo mjini Lusaka.
Mwili wa aliyekuwa Rais wa Zambia marehemu Michael Sata ukiwasili katika viwanja vya Bunge la Zambia tayari kwa misa Maalum iliyoandaliwa kabla ya mazishi kufanyika leo.
Mjane wa aliyekuwa Rais wa Zambia Dkt. Christine Kaseba Sata akiliwazwa na mke wa kaimu Rais wa nchi hiyo Bi. Charlote Scot wakati wa Misa hiyo.
kaunda akitafakari kwa huzuni kifo cha Sata.
Kutoka kushoto ni Dkt. Kenneth Kaunda, Rupia Banda na Anne Makinda wakiwa na huzuni tele.
MC akiongoza misa hiyo.
Makinda akihojiwa na Waandishi mara baada ya kumalizika kwa misa hiyo.
Rais wa Bunge la SADC na ambaye ni Spika wa Bunge la Tanzania akiondoka katika viwanja vya Bunge la Zambia na Mwenyeji wake Dkt. Patrick Matibini, Spika wa Bunge la Zambia. Picha zote na Owen Mwandumbya wa Bunge

No comments:

Post a Comment