Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis
Mwamunyange na IGP Ernest Mangu wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo
tayari kuanza ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China
kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mhe Raymond
Mushi wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza ziara
rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais
Xi Jinping.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagwa na maafisa wa Ubalozi wa China nchini
Tanzanioa wakati akiondoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Julius Nyerere jijini Dar es salaam usiku wa kuamkia leo tayari kuanza
ziara rasmi ya siku sita katika Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa
Rais Xi Jinping. PICHA NA IKULU
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete
leo, Jumanne, Oktoba 21, 2014, anaanza ziara rasmi ya siku sita katika
Jamhuri ya Watu wa China kwa mwaliko wa Rais Xi Jinping, ikiwa ni ziara
yake ya pili nchini humo akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Baada ya China, Rais Kikwete atafanya ziara rasmi ya siku tatu nchini Vietnam kwa mwaliko wa Rais wa nchi hiyo. Wakati wa ziara yake nchini China, Rais Kikwete ambaye aliondoka
nchini usiku wa jana, Jumatatu, Oktoba 20, 2014, atatembelea majimbo matatu ya nchi hiyo, atafanya mazungumzo na viongozi wakuu wa China, atashuhudia utiaji saini mikataba muhimu ya shughuli za maendeleo, atatunukiwa shahada za heshima na atashiriki katika sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na
China.
nchini usiku wa jana, Jumatatu, Oktoba 20, 2014, atatembelea majimbo matatu ya nchi hiyo, atafanya mazungumzo na viongozi wakuu wa China, atashuhudia utiaji saini mikataba muhimu ya shughuli za maendeleo, atatunukiwa shahada za heshima na atashiriki katika sherehe za miaka 50 tokea kuanzishwa kwa uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania na
China.
Rais
Kikwete amepangiwa kukutana na kufanya mazungumzo na mwenyeji wake,
Rais Xi Jinping; Waziri Mkuu Mheshimiwa Li Keqiang pamoja na Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Watu wa China, Mheshimiwa Zhang Dejiang. Rais
Kikwete pia atashuhudia utiaji saini wa mikataba ya miradi ya maendeleo
ya Tanzania ambayo inasaidiwa ama inagharimiwa na fedha kutoka China na
pia atakutana kwa mazungumzo na wakuu wa taasisi muhimu zinazogharimia
baadhi ya miradi mikubwa ya maendeleo katika Tanzania zikiwamo
China-Africa Development Fund (CADB) na China Development Bank (CDB).
Akiwa
Beijing, Rais Kikwete atakutana na Mabalozi wa Afrika wanaoziwakilisha
nchi zao katika China, atafungua Mkutano wa Tatu wa Biashara na
Uwekezaji kati ya Tanzania na China na atazindua rasmi Kijiji cha
Kiafrika.
Aidha,
Rais Kikwete atatunukiwa uprofesa wa heshima na Chuo Kikuu cha Kilimo
cha China cha China Agricultural University na Chuo Kikuu cha East China
Normal University na pia atakuwa mwenyeji wa hafla maalum ya
kusherehekea miaka 50 ya uhusiano wa kibalozi kati ya Tanzania
na China.
Uhusiano
huo ulitimiza miaka 50, Aprili 26, mwaka huu, siku ambako Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania pia ilitimiza miaka 50 ya kuzaliwa kwake.
Baada
ya kumaliza ziara yake Beijing, Rais Kikwete atatembelea Jimbo la Jinan
ambako atashuhudia maonyesho rasmi ya kijeshi ya Jeshi la Ukombozi la
Wananchi wa China la Chinese People’s Liberation Army (PLA)
lililoandaliwa rasmi kwa heshima yake. Hiyo itakuwa mara ya kwanza
katika historia kwa heshima ya namna hiyo kutolewa kwa kiongozi
wa nchi yoyote duniani, nje ya China.
wa nchi yoyote duniani, nje ya China.
Akiwa
Jimbo la Jinan, Rais Kikwete pia atakutana na viongozi wa Jimbo hilo na
pia atakutana kwa mazungumzo na madaktari wa Kichina ambao wamefanya
kazi katika Tanzania katika miaka 50 iliyopita.
Baada
ya Jimbo la Jinan, Rais Kikwete atakwenda Jimbo la Shenzhen ambako
atatembelea makao makuu ya taasisi na makampuni makubwa ya China ya
Shenzhen Economic Zones Authority, China Merchants
Holdings International (CMHI), Huawei na ZTE. Shenzhen ndiko Watanzania
wengi wanaonunua bidhaa kutoka China hufanyia biashara zao.
Mara
ya mwisho, Rais Kikwete alitembelea China mwaka 2008
wakati alipoliwakilisha Bara la Afrika katika Mkutano wa Kwanza
wa China-Afrika katika nafasi yake wakati huo kama Mwenyekiti wa Umoja
wa Afrika (AU).
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Oktoba,2014
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Oktoba,2014
No comments:
Post a Comment