Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya
Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John
Kahyoza akiwaeleza waandishi wa (hawapo pichani) mikakati iliyoweka iliyowekwa
na Mahakama ya Tanzania ili kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa wote na kwa
wakati kwa vitendo, kwa kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri kukaa
mahakamani, wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni
Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi. Mary Gwera. Picha na Hassan silayo-maelezo
Na Georgina Misama-MAELEZO.
Mahakama ya Tanzania imedhamiria kutekeleza dira yake ya haki sawa kwa
wote ili kuhakikisha inapunguza muda wa mashauri na rufaa kukaa
Mahakamani kwa muda mrefu.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Mahakama ya Tanzania Bi Mary Gwera wakati wa mkutano uliofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Akizitaja hatua zilizochukuliwa na Mahakama Bi Mary alisema, kuboresha
bajeti ya kushughulikia mashauri kupitia mfuko wa mahakama toka bilioni
57 kwa mwaka 2012/13 mpaka bilioni 88 mwaka 2014/15, Idadi ya vikao vya
Mahakama ya Rufani vimeongezeka kutoka 26 mwaka 2012 hadi 34 mwaka
2013/14.
Aidha, Bi Mary alisema kuwa hatua nyingine ni pamoja na kuanzisha
kitengo cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kitakachoshughulikia masuala ya
utatuzi wa mashauri kwa njia ya suluhu muafaka, pia uundwaji wa kamati
ya kanuni za Mahakama itakayosaidia kutunga au kurekebisha kanuni ili
kuhakikisha kuwa kanuni zinazotumika Mahakamani si chanzo cha kuchelewa
mashauri Mahakamami
Naye, Kaimu Mkurugenzi, Kurugenzi ya Usimamizi na Uendeshaji wa Mashauri
kutoka Mahakama ya Tanzania Bw. John Kahyoza alisema kuwa Mahakama
imeanza kuchukua hatua za kuimarisha ukaguzi wa shughuli za Mahakama na
maadili ya watumishi kwa kuanzisha kurugenzi ya ukaguzi na maadili.
Aidha, Bw Kahyoza alivitaja viwango ambavyo kila hakimu au Jaji
anatakiwa kuvitimiza kwa mwaka na muda ambao mashauri yanatakiwa kuwa
Mahakamani kuwa ni Mh. Jaji wa Mahakama Kuu analenga kumaliza kesi 220,
Mahakimu wa Mahakama za Wilaya na Hakimu Mkazi kesi 250 na Mahakimu wa
Mahakama za mwanzo kesi 260
Mahakama Kuu inatoa rai kwa Watanzania kufika Mahakamani kwa Tarehe
zinazopangwa ili kuisaidia Mahakama kuhakikisha inapunguza muda wa
mashauri kukaa Mahakamani.
No comments:
Post a Comment