Kiongozi
wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge
Duniani (IPU) Mhe. Hamad Rashid Mohamed akifatilia kwa makini Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU),unaofanyika mjini Geneva,Uswis.
Kiongozi
wa Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 131 wa Chama cha Mabunge
Duniani (IPU) Mhe. Hamad Rashid Mohamed akiteta jambo na Balozi wa
Kudumu katika Umoja wa Mataifa Geneva, Uswis, Balozi Modest Mero wakati
wa Mkutano wa chama hicho mjini Geneva leo.
Ujumbe
wa Tanzania ukiongozwa naMhe. Hamad Rashid Mohamed wakishiriki Mkutano
wa 131 wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) Mjini Geneva, Uswis.
Na Owen Mwandumbya, Geneva
Wabunge
kutoka Mabunge wanachama wa Chama cha Mabunge Duniani (IPU) wanakutana
Mjini Geneva Usiwisi katika Mkutano wa mwaka wa 131 wa chama hicho
kujadili na kutafuta ufumbuzi wa namna ya kukabiliana na baadhi ya
matatizo yanayoyakumba mataifa mbalimbali duniani ikiwemo usalama pamoja
na uvunjaji wa haki za Binadamu.
Katika
mkutano huo ambao unahudhuriwa na jumla ya wabunge 700 kutoka nchi
wananchama 141 wakiongozwa na Maspika na Manaibu spika kutoka nchi 104
umeanza jana tarehe 12 na unatarajiwa kumalizika ijumaa tarehe 16
Oktoba, 2014 kwa kufanya uchaguzi kumchagua rasi wa chama cha kibunge na
ambacho ni kikubwa Duniani.
Katika
agenda za mkutano huo, mojawapo ya masuala yanayojadiliwa ni pamoja na
kuja na suluhu ya kibunge ya namna ya kukabiliana na kubambana na ugaidi
duniani na masuala yote ya imani kali yanayopeleka kuleta machafuko
katika baadhi ya nchi hususani za kiarabu kwa kuangamiza maelfu ya watu
wasio na hatia. Pamoja na masuala hayo, wabunge hao pia wanajadili namna
bora ya nchi wanachama kuwa na sheria madhubuti ya kupiga vita biashara
haramu ya usafirishaji wa Binadamu, pamoja na kutambua uhuru wa kila
Taifa bila kuingiliwa na mataifa mengine.
Tanzania
katika Mkutano huo inawakilishwa na Wabunge wambao ni wanacham wa
kudumu katika mkutano huo ambao ni mhe. Hamad Rashid Mohamed, Mhe. Suzan
Lyimo na Mhe. Dkt. Pudensiana kikwembe.
Katika
mchango wa Tanzania, kiongozi wa Msafara wa Wabunge kutoka Tanzania
Mhe. Hamad Rashid Mohamed akichangia katika Mkutano mKuu w huo ameelezea
namna Tanzania inavyounga mkono jitihada za IPu katika kupiga vita
masula ya Ugadi ikiwa ni pmoja na jitihada za chombo hicho kutambua
uwakilsihi wa wanawake katika masula ya uongozi.
Akisisitiza
umuhimu wa mabunge kuwa na sheria rasmi zinazoweza kumlinda mwananke
katika ukatili wa kijinsia, Mjumbe kutoka Tanzania Mhe. Suzan Lyimo
amesema, takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa mwananmke mmoja katika kila
wanawake watatu hivi sasa ni mhanga wa ukatili wa kijinsia unaofanya
katika ngazi ya kifamilia na hata utawala hususani na machafuko ya
kivita. Ansema bila kujipanga vyema katika ngazi ya kibunge kuwa na
sheria na utaratibu madhubuti ya kumlinda mwananke, machafuko
yanayotokea duniani hivi sasa yatazidi kumwangamiza mwanamke .
Akitolea
mfano wa makundi hatari yanayotokea duniani hivi sasa kama vile ISIS,
BOKO HARAM, ambayo kwa kiasi kikubwa yamekuwa tishio kubwa kwa usalama
wa kimataifa bali hata kwa ustawi wa wanawake duniani kutokana na
vitendo vyao vya kuwadhalilisha wanawake.
Mkutano
huo unaendelea leo kwa kuangalia masula mengine ya kimataifa na namna
mabunge yote duniani yatasaidiana na Serikali zake kutatua migogoro hiii
ya kimataifa.
No comments:
Post a Comment