Robert
Muthami Program Support Officer kutoka Pan African Climate Justice
Alliance (PACJA) akitoa ufafanuzi juu ya baadhi ya mambo yanayohusu
mabadiliko ya Tabianchi.
Kulia
ni mmoja wa walalamikaji kutoka Loliondo akielezea kwa uchungu jinsi
Muwekezaji alivyo wanyang'anya Ardhi yao na mpaka sasa hakuna kitu
ambacho kinaendelea na wanahitaji kupata Msaada wa kisheria ili wapate
rudishiwa Ardhi yao.
Kulia
ni Mama kutoka Loliondo akitoa malalamiko yake Mbele ya Mahakama ya
wazi Jinsi mwekezaji alivyochukua Ardhi, kusababisha uharibifu na akina
mama kuteseka pamoja na wengine kuharibu Mimba zao pia kupoteza watoto
ambapo mpaka sasa kuna mtoto hajaonekana.
Mlalamikaji
Mwingine kutoka Loliondo akielezea Mbele ya Mahakama ya wazi jinsi ya
eneo lao lilivyochukulia na mwekezaji, na kutaka agizo la Mh. Waziri
Mkuu lifanyiwe kazi la kwamba ardhi ile ni ya wafugaji na wanatakiwa
warudishiwe
Mmoja
wa walalamikaji kutoka Wilaya ya Kishapu akitoa malalamiko yake mbele
ya Mahakama ya wazi juu ya walivyo chukuliwa maeneo kwa ahadi ya
kuyaendeleza na kuto fanya hivyo, na kuomba eneo hilo ambalo ni mashamba
warudishiwe ili waendelee na kilimo kwa kuwa eneo hilo kuna shida ya
njaa.
Mchangiaji
kutoka Oxfam Bwana Marc akizungumza juu ya haki za binadamu na moja ya
haki hizo ni haki ya kila mwanadamu kuwa na Chakula, na kuongezea kuwa
hata Umoja wa Mataifa unafahamu hilo Pia amesisitiza kuwa ni jukumu la
kila mtu kujua sheria za umiliki wa Ardhi
Mjumbe wa Bodi kutoka Forum CC akizungumza jambo wakati wa Mkutano huo
Mh. Jaji Richard Mziray Akitoa Maelezo ya kina juu ya Walalamikaji
kutoka Loliondo ambao walikuwa wana malalamiko ya Ardhi na Kishapu
ambapo walikuwa wanataka Eneo lao lirudishwe, Ametoa maelekezo ya yale
ambayo wanatakiwa wayafuate.
Washiriki wa Mkutano huo
Mama Shujaa wa Chakula 2014 akichangia maada
Burudani Elimisha ikiendelea
Wadau wameguswa na kujumuika kucheza
Picha ya pamoja
No comments:
Post a Comment