Wazalendo 25 Blog inakutakia Maisha marefu na Mungu akuzidishie Nguvu, Juhudi na Ubunifu katika maisha yako.
hizo ni kama Zeze, Mapozi, Seya na hata Zuwena.
USHAURI WA Mc PiliPili kwa Serikali
Pia anaishauri serikali kurudisha masomo ya sanaa na kuweka walimu maalum wanaojua sanaa kufundisha masomo hayo na kuwawekea watoto msingi mzuri wa kitu wanachokipenda kufanya tangu wakiwa wadogo kwani kila mtu ana kipaji chake na anasisitiza kuwa kazi ambayo mtu ataifanya vizuri na kwa ufanisi ni kazi ambayo anaioenda na ataifanya kutoka moyoni.
Emmanuel Mathias almaarufu kama Mc Pilipili mwenye
uso wa uchekeshaji kama kazi yake ilivyo, alizaliwa mtaa wa Airport Dodoma
mjini mnamo tarehe 1 mwezi wa 10 mwaka 1985 akiwa ni mtoto wa pili wa Bwana Mathias
Matebe na Bi Mariam Matebe.
Emmanuel
alianza elimu yake ya shule ya msingi katika shule ya msingi Kiwanja cha Ndege
ambapo alisoma mpaka darasa la nne na kuhamia shule ya msingi Ipagala ambako
alimalizia elimu yake ya msingi hapo mnamo mwaka 2000.
Akiwa shule ya msingi Emmanuel kijana mdogo na
mcheshi alijihusisha na masuala ya uchoraji, uimbaji na hata kucheza muziki
ingawa alikua na ndoto za kuwa Muandishi wa habari.
“mimi nilivutiwa saana na kazi za waaandishi wa
habari na nikatamani sana siku moja niwe muandishi wa habari kama wao, japo
nilikuwa pia natamani kuwa Mchungaji”. Alielezea kwa Emmanuel kwa kukumbuka.
“Nkumbuka nikiwa na umri wa miaka nane, ilikuja
bendi ya Afriso iliyokuwa chini ya Super Lovii Longomba, kaka wa Awilo
Longomba, daah! Nilitunzwa hela nyingii na ndio ilikuwa hela yangu ya kwanza
ambayo pia niliitumia kulipa kodi ya nyumba tuliokuwa tunadaiwa na pia
kununulia debe la unga kwani kwa kipindi hicho baba yangu alikuwa muuza
mishkaki na mama alikuwa anauza ndizi hospitali hivyo hawakuweza kwa kipindi
hicho kulipa kodi hali iliyopelekea kutaka kufukuzwa tulipokuwa tunaishi,
ilitusaidia sana”.
Akiwa bado na umri mdogo, aliweza pia kuigiza sauti
mbalimbali kama ya mwalimu Nyerere, Mwakasege, Mr. Bean na pia kubadili nyimbo
za wasanii mbalimbali wa kizazi kipya na
kuziimba kwa Kigogo. Nyimbo
Emmanuel aliweza kutunukiwa cheti cha ‘MTOTO WA
NURU’ kama mtoto wa mfano na wa kuigwa katika kanisa la Baptist Bible Church
ambapo alikuwa akisali na familia yake.
Baaada ya kumaliza darasa la saba Emmanuel alijiunga
na Shule ya sekondari Dodoma (Dodoma sekondari) mwaka 2001 ambapo ndoto zake za
kuwa muandishi wa habari zilipoanza kufunikwa taratibu.
Akiwa sekondari kama ilivyo kawaida huwa kuna masomo ya kuchagua, kutokana na
tabia yake, mwalimu Kilela ambaye sasa ni marehemu alinishauri nichukue somo la
‘Theatre arts’ ambalo ni la Sanaa ya jukwaani somo ambalo alilipenda na kufaulu
kuliko masomo mengine.
“Ilifikia hatua kila ninachoongea au watu
wakiniangalia tu wanacheka, mpaka darasani ilifika hatua nikinyoosha mkono
kujibu swali mwalimu hanichagui anajua ntachekesha tu”.
Emmanuel alipendelea masuala ya sanaa hali
iliyopelekea kipaji chake cha uchekeshaji kukua na hata kuanza kuwa mshereheshaji
(MC) katika matukio mbalimbali kama Birthday, Sendoff, Harusi na hata Vipaimara
na baadaye kutunukiwa cheti cha ‘SPECIAL TALENT’ ama kipaji maalum alipohitimu kidato cha nne.
Aliendelea na kazi ya Ushereheshaji hata alipofika
kuanza masomo ya kidato cha Tano na Sita katika Shule ya Sekondari Jubilee
mkoani Dodoma.
Baada ya kuhitimu kidato cha Sita, Emmanuel alipata
ufadhili kutoka kwa wahisani ambapo alipaswa kwenda kusomea Ualimu.
“nilipata wakati mgumu sana kufanya uamuzi kwani
nilipenda kuwa Mwandishi wa habari na wakati huo huo mama yangu alisisitiza
niende ualimu kwani hata katika Familia yetu tu hakuna hata mmoja aliyewahi
kuwa mwandishi wa habari”.
Emmanuel alikubali kwenda katika Chuo cha Ualimu
Eckenforde kilichoko mkoani Tanga.
Alipofika chuoni hapo alipata changamoto ya
kusitisha tabia yake ya Uchekeshaji kwani alionywa na familia yake kuwa makini
kwani amefadhiliwa hivyo akazane na kitu alichofuata chuoni.
“Kwakweli nilipata shida sana kwani hata nikisimama
kimya mbele za watu walikua wanaangua vicheko wengine mpaka wanatoka machozi”.
Alihadithia Emmanuel.
Waswahili husema, Maji ukiyavulia nguo sharti
Uyaoge. Emmanueli au MC Pilipili alijikuta akiyaoga maji ya Uchekeshaji kwani
alijikuta akianza kusherehesha katika Matamasha mbalimbali ya kidini ndani na
nje ya Chuo.
“Kila palipotokea matamasha ya kidini kama Joint
mass au Graduation walinichagua kuwa MC na watu walikuwa wakisikia ni mimi
ntaogoza walifurahi na kujaa kwa wingi. Nilipata fursa ya kutembelea mikoa
mbalimbali kwa kazi hii kama Dar es salaam na Morogoro”.
Mnamo mwaka 2009 Emmanuel alihitimu mafunzo yake ya
Ualimu chuoni hapo na kupangiwa kufanya kazi Mkoani Manyara.
“Lakini sikupenda mkoa ule kwa sababu hauna sherehe
nyingi kwahiyo nikaona kazi yangu ya uchekeshaji na uMC itakuwa ngumu kuifanya,
ikabidi niombe kufundisha katika shule niliyosoma kidato cha tano na sita na
walinipokea tayari kwa kazi ya ualimu hapo”.
.
Mwaka huo wa 2009 Emmanuel alijikuta ana majukumu makubwa ya kuhudumia familia kwani kwa kipindi hicho
baba yake mzazi alikuwa mgonjwa hivyo mama ambaye kwa wakati huo alikuwa ni
mwalimu katika shule moja ya chekechea mjini hapo alikuwa anamuuguza baba
nyumbani.
“Kwa bahati mbaya tarehe 30/5/2009 nilimpoteza baba
yangu mzee Mathias Mtebe, niliumia sana kwani tulibaki sisi na mama peke yetu.
Niliendelea kutafuta hela nyingi zaidi
kwani kwa kipindi hicho familia yangu ilikuwa inanitegemea kwa kila kitu kama
baba”.
Aliajiriwa rasmi shuleni Jubilee sekondari mwezi wa
7 mwaka huo huo na kendelea na kazi ya ualimu kama mwalimu wa msomo ya
Kiswahili, Historia, Bible knowledge pamoja na Civics.
Emmanuel ambaye kwa kipindi hicho jina la MC
Pilipili lilikuwa tayari limeshajulikana zaidi kwa watu, aliendelea na kazi
yake ya Uchekeshaji na Ushereheshaji kwa mapana zaidi kwani alikuwa na uwezo wa
kusafiri kwenda mikoani.
Mwaka 2013 tarehe 30 mwezi wa 1, Pilipili aliacha
rasmi kazi ya ualimu na kujishughulisha moja kwa moja na kazi ya Uchekeshaji na
Ushereheshaji kazi ambayo ilimuingizia kipato zaidi akiilinganisha na ualimu.
“Baada ya kuwa nasafiri sana kuja Dar na kurudi
Dodoma nilijikuta kwakweli nakuja zaidi ya mara moja kwa wiki na kwa bahati
nzuri kipato cha Ushereheshaji kilikuwa kinazidi kabisa kile cha ualimu”.
Anaendelea kusema kwamba hakuwa na jinsi zaidi ya kusitisha ualimu.
Mgaagaa na Upwa hali wali mkavu. Pilipili aihamia
Dar es salaam ambapo ssa alifanya kazi
hiyo rasmi na kwa ufanisi mzuri.
“Yaani naweza nikapata ‘deal’ nyingi kwa wiki nzima
mfululizo ila sio chini ya mara mbili kwa wiki na kila kazi huwa natoza si
chini ya Shilingi miliomi mija na laki nne kama mtu atanihitaji kama MC na
Mchekeshaji. Ukiniita kama mchekeshaji peke yake una MC wako huwa inakuwa kama
Shilingi laki nane hivi ambapo kwa Ushereheshaji peke yake ni kama million moja
na laki mbili hivi.
MC Pilipili anaelezea kuwa mafanikio aliyoyapata
kutokana na kazi hii ni makubwa sana kwani ameweza kujenga nyumba kubwa mbili
nyumbani kwao, anamiliki viwanja vitano pamoja na akiba ya kutosha kwa matumizi
yake ambayo iko Benki.
Kwa upande wa changamoto Pilipili anasema “Kwakweli
kazi hii ni ya imani, unaweza ukaamka hujui hata utafanya nini wiki nzima
lakini zikafululizana simu unapigiwa kuwa unahitajika, unabaki kupanga wewe
sasa uende wapi’. Pia anaendelea kusema kuwa sanaa ya uchekeshaji kwa Tanzania
bado haijakubalika sana haswa uchekeshaji wima (Stand up Comedy)
Pilipili ameweza kufanya kazi ya Uchekeshaji na
Ushereheshaji katika nchi mbalimbali kama Kenya, Rwanda, Uganda pamoja na Afrka
ya kusini hali iliyomsaidia kujitangaza ndani nan je ya nchi kwani mashirika na
kampuni mbalimbali humwita sana kuongoza sherehe na matukio mbalimbali.
“Matarajio yangu ni kutangaza Stand up comedy
Tanzania pamoja na sanaa ya uchekeshaji na pia kuitangaza Tanzania kupitia
Stand up comedy”.
Pilipili ambaye bado ni kijana anawasihi vijana
wenzake kutumia vipaji vyao na sio kulazimisha usomi. Anasema, “Kipaji kinaweza
kukupeleka mbele ya wakuu” akitolea mfano wa watu wa kwenye Biblia kama Mfalme
Daudi na Yusuph ambao walitumia vipaji vyao na wakainuliwa na Mungu.
Pilipili
ameweza kualikwa Bungeni ambapo alitambulishwa kama mchekeshaji wa Tanzania,
Kualikwa Makanisa mbalimbali kutoa mafunzo na mahubiri na pia alifanya kazi
jukwaa moja na Eric Omondi kutoka Kenya mwezi wa 12 mwaka 2013 katika hoteli
Golden Tulip kama wachekeshaji.
“Npenda kutumia usemi unaosema ‘Sherehe ni Mc”.
Aliyasema hayo akiwasahauri washereheshaji wenzake kufanya kazi hiyo kwa
kuhakikisha wanasoma vitabu, kuangalia internet kuona nini wanatakiwa kufanya
pamoja na kuwa na Usasa ili wafanye kazi
hiyo katika kiwango kizuri.
Pia anaishauri serikali kurudisha masomo ya sanaa na kuweka walimu maalum wanaojua sanaa kufundisha masomo hayo na kuwawekea watoto msingi mzuri wa kitu wanachokipenda kufanya tangu wakiwa wadogo kwani kila mtu ana kipaji chake na anasisitiza kuwa kazi ambayo mtu ataifanya vizuri na kwa ufanisi ni kazi ambayo anaioenda na ataifanya kutoka moyoni.
No comments:
Post a Comment