Ofisa
Uhusiano wa Siku ya Msanii Tanzania (SYM), Bw. Peter Mwendapole
akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Siku ya Msanii Tanzania
itakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City siku ya tarehe 25 Oktoba,
2014 jijini Dar es Salaam.
Mwimbaji wa muziki wa taarabu, Bi. Isha
Ramadhan maarufu kama Mashauzi akiongea na waandishi wa habari kuhusu
Siku ya Msanii Tanzania itakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City
siku ya tarehe 25 Oktoba, 2014 jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA MAGRETH KINABO, MAELEZO
**************************************
Na Beatrice Lyimo- Maelezo.
KAMATI
ya Siku ya Msanii Tanzania (SYM) imetangaza rasmi majina ya wasanii
watakaotumbuiza katika maadhimisho ya siku hiyo itakayofanyika Oktoba 25
mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City uliopo jijini Dar Es Salaam.
Akizingumza na waandishi wa habari leo jijini Dar Es Salaam, Ofisa Uhusiano wa SYM, Bw.
Peter Mwendapole amesema kuwa, kutokana na siku hiyo kuwa ni ya Sanaa
zote, Kamati imeangalia uwakilishi wa sanaa za aina mbalimbali ili
ziweze kuwakilisha siku hiyo katika historia ya Tanzania.
“Leo
tungependa kuwatangaza Wasanii watatu wa Bendi ya Kilimanjaro Wana
Njenje wenye vionjo vya Tanzania na Wawakilishi wa kundi la Wanamuziki
wakongwe”, alisema Mwendapole.
Mwendapole
alisema kuwa, kwa upande wa sanaa kuatkuwa na msanii maarufu kama Isha
Mashauzi ambaye atawakilisha fani ya muziki wa jukwaani na upande wa
Taarabu, kwani msanii huyo ameweza kufanya mapinduzi makubwa kwenye
muziki wa taarabu pamoja na kuweka vionjo mbalimbali vya dansi, asili na
taarabu.
Aliongeza
kuwa, kutakuwa na kikundi cha sanaa kijulikanacho kama Ako Mpiruka
Sound, bendi ya muziki, kikundi cha ngoma, kikundi cha sarakasi, wacheza
Yoga na pia kutakuwa na shoo ya muziki wa dansi pamoja na dansi za
mitaani.
Amebainisha
kuwa, vijana wanaocheza muziki mitaani wakiwezeshwa wanaweza kujiajiri
na kupunguza idadi kubwa ya watu ambao hawana ajira.
“Siku
ya msanii tunataka kuonyesha jinsi gani wanenguaji wana uwezo wa
kucheza bila ya kuonyesha maungo yao”, alisisitiza Mwendapole.
Akifafanua
kuhusu kiingilio cha siku hiyo ya msanii alisema kuwa, kiingilio hicho
kitakuwa ni shilingi 70,000 kwa VIP na 50,000 kwa viti vya kawaida.
Siku
ya msanii inaandaliwa na kampuni Haak Neel Production (T) Ltd kwa
kushirikiana na Baraza la Sanaaa la Taifa (BASATA) na kudhaminiwa na New
Habari (2006) LTD kupitia magazeti ya Bingwa, Dimba, The African, na
Mtanzania.
Wadhamini
wengine wa SYM pamoja na PSPF, Azam Media, EFM, Magic FM, Clouds FM,
Channel Ten, CXC, Ledger Plaza Hotel pamoja na Proin Tanzania.
No comments:
Post a Comment