Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi wa kata ya
Kwaluguru wakati wa kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vitatu vya
maabara katika shule ya sekondari Kwaluguru wilayani Handeni.
Wananchi
wa kata ya Kwaluguru wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahma
Kinana wakati wa ukaguzi wa maendeleo ya ujenzi wa maabara tatu za
masomo ya sayansi katika shule ya sekondari Kwaluguru ambapo vyumba 83
vya maabara vinajengwa wilayani Handeni.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wakazi wa Handeni kwenye uwanja wa mkutano Soko la Zamani Chanika.
Mwenyekiti
wa CCM mkoa wa Tanga Henry Shekifu akisalimia wakazi wa Handeni kabla
ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuhutubia.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Handeni
ambapo aliwaambia watu wanatakiwa kupewa fursa na kurahisishiwa maisha
yao hivyo kodi ndogo zinatakiwa ziangaliwe upya kwani zimekuwa kero kwa
wafanyabiashara ndogo ndogo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na madereva wa boda boda wa Chanika Handeni
Watu wakiwa wamemzunguka Katibu Mkuu wa CCM mara baada ya kumaliza mkutano wake Soko la zamani Chanika wilayani Handeni.
No comments:
Post a Comment