Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto)
akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini Bw.Richard Ragan
(katikati) pamoja na Mwakilishi wa mkazi wa shirika la Afya Duniani
(WHO) Dk Rufaro Chatora (kulia) kabla ya kuanza kwa mkutano wa kuboresha
ushirikiano kati ya Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na wahariri wa
vyombo mbalimbali vya habari nchini.
Shirika
la Umoja wa Mataifa nchini UN lakutana na wanahabari kujadiliana na
kudumisha ushirikiano wao katika habari ambapo wahariri wa vyombo
mbalimbali vya habari wamekuna na viongozi mbalimbali wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa ili kujadili kwa pamoja.
UN
wameeleza kazi zinazofanywa na shirika hilo ili waweze kushirikiana
kwenye mambo mbalimbali katika kuhakikisha wananchi wanapata taarifa
sahihi, elimu na kuzifahamu kazi za mashirika hayo hapa nchini.
Hivyo
waandishi na wahariri wa habari wameombwa kudumisha ushirikiano katika
kazi zote zinazofanywa na mashirika yanayosaidia nchini kwa kiasi
kikubwa.
Pia wameweza kuzungumzia ugonjwa wa Ebola ambao umeibuka kwa kasi sana
hivyo kuwataka kuweza kuandika habari zinazowajuza jamii ili kuweza
kuuepuka.
Nia
na madhumuni ya mkutano huo na wahariri wa vyombo vya habari ni kuweza
kujenga ushirikiano madhubuti baina yao na kuweza kushirikiana kwa
karibu katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa nchini (UNDP) Bw.
Phillippe Poinsot akijibu moja ya maswali yaliyoulizwa wakati wa mkutano
huo.
Picha
ya pamoja mara baada ya mkutano wa kuboresha mahusiano na wahariri wa
vyombo mbalimbali vya habari pamoja na mashirika ya umoja wa mataifa
nchini.
No comments:
Post a Comment