Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Marie Stopes Tanzania (MST), Uller Muller (kulia)
akikabidhi kisanduku chenye vifaa vinavyohusika na masuala ya uzazi wa
mpango kwa Balozi mpya wa Marie Stopes ambaye pia ni msanii mkongwe wa
muziki wa kizazi kipya, Judith Wambura 'Lady jaydee' katika hafla ya
utiaji saini makubaliano hayo katika ofisi za MST, jijiji Dar es Salaam.
MSANII
wa muziki wa kizazi kipya Judith Wambura 'Lady Jaydee', ameteuliwa kuwa
Balozi mpya wa Marie Stopes,katika kampeni za uzazi wa mpango.
Akitangazwa
rasmi kuwa balozi mpya msanii Jay Dee aliibua shangwe na nderemo
zilizotoka kwa baadhi ya wazazi na watu waliohudhuria hafla hiyo
iliyofanyika kwenye Ofisi za MST zilizopo Mwenge jijini Dar es Salaam.
Jay
Dee sasa anaungana na Marie Stopes kwenye kampeni ya “Chagua Maisha”
ambayo inalenga kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango
katika jamii.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kutangazwa rasmi, Jaydee alisema kuwa
amefurahi sana kupata nafasi hiyo ambayo anaamini ataitendea haki
kulingana na nafasi yake kwa jamii.
“Nina
furaha kubwa kuchukuka nafasi hii ya kipekee kama Balozi wa Marie
Stopes kwa sababu wanafanya mengi kuwawezesha kina mama kusimama na
kujitegemea, na pia naamini nitafanya kazi nzuri kwa ushirikiano na
Marie stopes ili kuiwezesha Jamii kufikia na kuelewa vyema lengo la
Uzazi wa mpango''. alisema Jay dee
Lengo
kuu la Kampeni hii ya Chagua Maisha nikuhakikisha kila Mtanzania ana
haki ya kuchagua mfumo wa uzazi wa mpango ili kulinda afya zao na
kutimiza malengo yao ya kimaisha, hususan mabinti wadogo”.
Akitafakari
sababu zilizompeleka kuungana na kampeni hii, Lady Jaydee alieleza:
“siku zote nilikuwa naamini kuwa wanawake wana uwezo wa kubadilisha
Tanzania kimaendeleo. Hivyo niliumizwa moyo sana nilipoambiwa hivi leo
kuwa Wanawake wengi hupoteza maisha, na wasichana wengi wanalazimishwa
kuacha masomo kutoka na ujauzito. Mimi nimeamua kusaidiana na Marie
Stopes kuelimisha jamii nzima wanaweza kubalili fikra na hatima zao, kwa
kutumia uzazi wa mpango”.
Takwimu
zinaonyesha kuwa Tanzania ni nchi inayoongoza kwenye idadi ya vijana,
54% wakiwa chini ya umri wa miaka 20. Vijana hawa wana uwezo wa
kubadili na kukuza hali ya kiuchumi ya Tanzania ndani ya miaka 10 ijayo
iwapo watapata msaada.
Akiwa
amesimama Pamoja na Lady Jaydee, Bi Muller alikuwa na haya ya kusema:
“Leo hii nchini Tanzania, mmjoa kati ya kila Wanawake wane chini ya umri
wa miaka 19 wamekwisha kuwa wazazi na asilimia 20% ya Wanawake chini ya
umri wa miaka 20 wamo katika ndoa za kulazimishwa.
Zaidi
ya hayo, kama binti akipata ujauzito hata kwa kubakwa, anafukuzwa shule
na huo ndio unakuwa mwisho wa elimu yake. Haya siyo mazingira mazuri
ambayo vijana wetu wanahitaji iwapo wana matumaini ya kukuza uchumi wa
taifa letu na kuliweka kuwa katika kipato cha kati (middle income).
Wanawake wana uwezo mkubwa wa kuchangia kukua kwa taifa letu, hivyo ni
jukumu letu kuwapa fursa hizo”.
“Nina
imani kubwa kuwa tutafanikiwa”, aliongeza Lady Jaydee, “tunataka kila
mmoja atambue kuwa ana haki ya kuchagua muda na wakati wa kupata watoto,
na pia idadi ya watoto wanaowataka. Marie Stopes na taasisi nyingine
zinaweza kukusaidia kumaliza masomo yako na kuhakikisha kuwa una maliza
elimu na kuwa na mwanzo mzuri wa maisha, kabla hujaamua kuwa mzazi. Name
nitaanza kueneza ujumbe huu Jumamosi hii kwenya Nyama Choma Festival,
Dar es Salaam!”
Tukio
hili la Lady Jaydee kutembelea Hospitali ya Marie Stopes jijini Dar es
Salaam litaonyeshwa jumapili tarehe 07 Septemba kwenye East Africa TV.
Kituo hiki kilichopo Mwenge ni miongoni mwa hospitali 11 za Marie Stopes
nchini Tanzania. Zote hizi zinatoa huduma za uzazi wa mpango kwa
Wanawake bure kabisa bila malipo yoyote.
No comments:
Post a Comment