MFUKO WA JAMII :SHEREHE YA MWAKA YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF YAFANA JIJINI DAR - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 22 September 2014

demo-image

MFUKO WA JAMII :SHEREHE YA MWAKA YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF YAFANA JIJINI DAR

Dr.Aggrey+Mlimuka+Kaimu+Mwenyekiti+wa+Bodi+ya+wadhamini+wa+Mfuko+wa+Pensheni+wa+PPF.
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akizungumza na wafanyakazi wa mfuko wa pensheni wa PPF wakati wa sherehe ya Mwaka iliyofanyika katika Ukumbi wa Blue Pearl Ubungo Jijini Dar Es Salaam Mwishoni mwa wiki.
IMG_0800
 Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka akiwapongeza Vijana wanaounda kundi la The Voice ambao ni wasanii wa fani ya Akapela mara baada ya Kutoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Ubungo Jijini Dar Es Salaam.
IMG_0776
Kundi la The Voice likitoa burudani katika sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl.
IMG_0723
Baadhi ya wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakifuatilia matukio yaliyokuwa yakiendelea katika Sherehe ya Mwaka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Ukumbi wa Blue Pearl.
IMG_0886
Afisa Mahusiano wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bi Janeth Ezekiel akipokea cheti na zawadi kutoka Kwa Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Udhamini wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Dr Aggrey Mlimuka mara baada ya kutangazwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2013 kutoka Idara ya Mahusiano na Masoko ya Mfuko wa Pensheni wa PPF katika sherehe ya mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar Es Salaam
IMG_0845
IMG_0849
IMG_0869
IMG_0865
 Pichani Juu Ni baadhi ya wafanyakazi kutoka Idara Mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PPF waliojipatia zawadi kwa kuwa wafanyakazi bora wa Mwaka 2013.
IMG_0811
Wafanyakazi wa PPF wakifuatilia Burudani iliyokuwa ikitolewa na Kundi la The Voice katika Sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika mwishoni mwa Wiki katika Hotel ya Blue Pearl.
IMG_0793
Mmoja wa wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF akimtunza Mmoja ya waimbaji wa kundi la the voice lililokuwa likitoa burudani wakati wa sherehe ya Mwaka ya Mfuko wa Pensheni wa PPF iliyofanyika Mwisho mwa Wiki katika hoteli ya Blue Pearl, Jijini Dar 
ppf
Wadau wakiserebuka Muziki mara baada ya wafanyakazi bora kupewa motisha na zawadi zao katika sherehe ya Mwaka ya PPF iliyofanyika Mwishoni mwa Wiki katika Hoteli ya Blue Pearl, Ubungo Jijini Dar Es Salaam.Picha zote na Josephat Lukaza.

No comments:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *