Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (wa
kwanza kulia) akitoa maelezo kuhusiana na maendeleo ya Bunge hilo wakati
alipotembelewa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma. Katikati ni Mjumbe wa Bunge
hilo, Mhe. Yassmin Alloo na kushoto ni Sheikh Hemed Jalala.
Baadhi ya Waandishi wakifuatilia
mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na mgeni wake Sheikh
Hemed Jalala 03 Septemba, 2014 mjini Dodoma.
Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akikabidhi kitabu kwa
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (kulia), kinachoitwa ‘Kilele cha Fasaha’ kinachohusu
maadili na uongozi.
Sheikh Hemed Jalala (kushoto) akiongoza dua ya kuiombea Bunge
Maalum la Katiba. Kulia ni Mwenyekiti wa Bunge hilo, Mhe. Samuel Sitta na
katikati ni Mjumbe wa Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta (wa
tatu toka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Sheikh Hemed Jalala (wa pili
toka kushoto) pamoja ujumbe aliofautana nao. Wa kwanza kulia ni Alhaj Mohamed
Mputa, anayemfuatia ni Sheikh Mohamed Abdi na wa tatu toka kulia ni Mjumbe wa
Bunge hilo, Mhe. Yassmin Alloo. Picha zote na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma
**************************************
Na Magreth Kinabo, Dodoma.
BAADHI ya viongozi wa dini wamempongeza Mwenyekiti wa
Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kwa kitendo chake cha kuliendesha Bunge hilo vizuri katika hali ya utulivu na amani.
Kauli hiyo imetolewa leo na Sheikh Hemed Jalala kutoka Msikiti wa Ghadiir
uliopo maeneo ya Kigogo Post jijini Dares Salaam, ambaye aliambatana na Masheikh
wengine ambao ni Alhaji Mohamed Mputa, Sheikh
Mohamed Abdi na Masoud Mbilili.
Aidha Sheikh Jalala akizungumza kwaniaba ya viongozi
wenzake wa dini alisema kuwa wamekuja kutembelea Bungeni hapo kwa ajili ya kumshukuru
Mhe. Sitta na kumuunga mkono kwa kazi nzito nzuri anayoifanya huku akisisitiza kuwa
wako nyuma yake katika suala hilo.
“Pamoja na changamoto zilizojitokeza
umeweza kukabiliananazo vizuri. Sisi na wananchi kila tunapolifuatilia tunaona mmeweza
kulipeleka vizuri. Jambo hili ni zito linahitaji amani, utulivu na kuvumiliana,”
alisema Sheikh Jalala.
Sheikh Jalala alisema wao
kama viongozi wa dini, wameona kuna changamoto ya maadili hivyo, wameandaa kitabu
maalum kinachoitwa ‘Kilele cha Fasaha’.
Alisema kitabu hicho kitasaidia
kutoa mchango wao kwenye masuala ya uongozi na maadili, ambacho alikikabidhi kwa
Mhe. Sitta.
Akipokea kitabu hicho,
Mhe.Sitta amesema ni jambo la baraka kwake, ambapo aliahidi kutoa taarifa juu ya
jambo hilo na kukikabidhi kitabu hiko katika Kamati ya Uongozi wa Bunge hilo.
Sheikh Jalala alisema
kuna jumla ya nakala 632 ya vitabu hivyo na vimeshakabidhiwa kwenye ofisi ya
Mwenyekiti wa Bunge hilo.
No comments:
Post a Comment