Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kutembelea banda la Shirika la
Bima la Taifa (NIC) katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani yaliyofanyika kitaifa jijini Arushaa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid, ,aliyeshika mice ni meneja wa shirika hilo Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin Ole Kambaine
Meneja
wa Shirika la Bima la Taifa (NIC)Mkoa wa Arusha na Manyara Bw.Godwin
Ole Kambaine akitoa maelezo mafupi kuhusu shirika hilo kwa Mkuu wa
wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa mara baada ya kutembelea
banda hilo jijini Arusha katikati ni meneja masoko na utafiti wa
shirika hilo kutoka makao makuu Bw.Elisante Maleko
Mdau
aliyetembelea banda hilo la Shirika la Bima la Taifa (NIC) akiwa
anauliza maswali yanayohusu shirikika hilo lengo nikutaka kufahamu zaidi
shughuli za shirika,kushoto ni Afisa wa Bima Bi.Costancia
Komanya
Meneja
masoko na utafiti wa shirika la Bima la Taifa (NIC) kutoka makao makuu
Bw.Elisante Maleko akiwa anatoa ufafanuzi kwa mdau aliyefika katika
banda lao ambapo alisema kuwa pamoja na bima nyingine pia wanatoa huduma
ya bima ya matibabu (madecare) ambao ni mpango maalum wa shirika hilo
kutoa matibabu kwa wananchi wa kada zote itakapotokea kaumwa na michango
ni midogo
Muonekano wa banda la shirika la Bima la Taifa (NIC) katika
maadhimisho ya wiki ya
nenda kwa usalama barabaranijijini Arusha
Meneja
masoko na utafiti wa shirika la Bima la Taifa (NIC) Bw.Elisante Maleko
amewataka watanzania kuona shirika hilo ni mali yao kwa kuwa shirika
hilo ni mali ya umma na michango ni midogo hivyo kila mwananchi
kumudu
Aliyasema
hayo jana wakati akizungumza na wadau mbalimbali waliyotembelea banda
lao katika maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani
yanayofanyika kitaifa katika uwanja wa Sheikh Amir Abeid jijini Arusha
Bw.Maleko
alisema kuwa shirika hilo lina bima ya matibabu amabayo ni mpango
maalum wa shirika hilo kutoa kinga ya matibabu kwa wananchi wa kada zote
itakapotokea kuumwa na michango ni
midogo na kila mwananchi anamudu kujiunga na huduma zinapatikana nchi
nzima
Pia
alisema Bima za nyumba inakinga na majanga ya wizi,moto,tetemeko na
mafuriko hivyo kuwataka wananchi kukatia nyumba zao bima. Picha na
Pamela Mollel wa jamiiblog
No comments:
Post a Comment