Waandishi wa habari wakirekodi tukio la kuwasili kwa Mh. Freeman Mbowe (hayuko pichani) Makao Makuu ya Polisi.
Mh. Tundu Lissu akiwasili. Mbuge wa Ubungo, Mh. John Mnyika akiwa ndani ya gari baada ya kukataliwa kuingia. Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema Mh. Wenje (kushoto), Mh. Msigwa na Mh. Joseph Mbilinyi wakiingia katika jengo hilo. Mwandishi wa habari Shamim Ausi mmoja wa wanahabari walioumia na kupoteza fedha na mali nyingine. Wanachama wa Chadema wakiwa wamekalishwa chini na askari. Kina mama ambao ni wanachama wa Chadema waliofika makao makuu ya polisi. Polisi wakiwakimbiza waandishi wa habari (hawako pichani) kwa kutumia mbwa. Wanahabari wakiwa wamekusanyika baada ya kutimuliwa na mbwa wa polisi. Mmoja wa wanachama wa Chadema, Kamugisha Ngaiza, alivyowekwa chini ya ulinzi na polisi. Muonekano wa polisi katika tukio hilo. Askari wakiwa hawataki kuwaona wanahabari eneo hilo. Mwandishi wa habari, Badi, akilia kwa uchungu baada ya kuumizwa na mbwa wa polisi.
- MNYIKA, WANASHERIA WAZUIWA KUINGIA NDANI
MAMIA
ya watu wamejitokeza leo kumsindikiza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, baada ya kuhitajiwa
kufika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi nchini, jijini Dar es Salaam
kuhusiana na kauli yake aliyotoa majuzi juu ya kuitisha maandamano nchi
nzima kupinga kuendelea kwa Bunge Maalum la Katiba.
Kilichofuata
ni polisi kuamuru watu wote waondoke eneo hilo kwa umbali wa mita 200
ambapo walikimbizwa na mbwa wa polisi na kusababisha wengi wao waumie na
kupoteza vitu vyao mbalimbali, hususani wanahabari ambao baadhi yao
waliumia na kupoteza zana zao za kazi.
(Habari/Picha na Gabriel Ng’osha/GPL)
No comments:
Post a Comment