Mkuu wa Kitengo Cha Mawasiliano, Wizara ya Fedha, Ingiahed Mduma (wa pili kushoto) na Kassim Kobelo Mkuu wa Hazina ndogo Mkoa wa Lindi ( wa pili kulia) wakiwa wameshika cheti cha ushindi wa pili wa maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yaliyofanyika Ngongo, Mkoani Lindi hivi karibuni. |
Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Fedha, Ingiahed Mduma akiwa na baadhi
ya watumishi katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa cheti cha
ushindi wa Maonyesho ya Kitaifa ya Nanenane yaliyofanyika Ngongo,
Mkoani Lindi hivi karibuni.
|
KATIKA
maonesho ya wakulima maarufu kama Nanenane yaliyomalizika hivi karibuni
kitaifa mkoani Lindi, Wizara ya Fedha ilishika namba mbili katika
taasisi zinazotoa huduma kwa wananchi nyuma ya Jeshi la Magereza.
Kilichoifanya
Wizara hiyo kushika nafasi hiyo ni kutokana na kutoa elimu muhimu kwa
wakulima kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu fedha na uchumi wa nchi
yetu, pamoja na maboresho ambayo yanaendelea serikalini.
Kila
idara, kuanzia kwenye Ofisi ya Mhasibu Mkuu hadi kwenye idara za
zinazohusika na pensheni, wananchi, kwa maana ya wakulima, walijifunza
mengi kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo wizara hiyo.
Kwa,
mfano katika ofisi ya Mhasibu Mkuu, wengi walijua kwamba, kama unafanya
kazi serikalini na kutunza kumbukumbu vizuri, unalipwa stahiki zako
mapema sana.
Hata
hivyo, katika makala haya tunaangalia idara moja wapo ambayo ilitoa
elimu kwa wananchi waliofika kwenye maonesho hayo, namna ambavyo imekuwa
ikifanya maboresho mbalimbali katika kusimamia fedha za umma. Hii ni
Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (PFMRP)
Mtu
ambaye alifika kwenye idara hiyo, aligundua mengi ikiwa ni pamoja na
mchango wa PFMRP katika ujio na utendaji madhubuti wa sasa wa Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ujio wa Mamlaka ya Uthibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA)
na kwamba mkakati unafanywa katima kuhakikisha serikali za mitaa
zinapunguza utegemezi wa kibajeti kwenye serikali kuu kwa kuweza
kukusanya mapato makubwa zaidi. Kwa sasa serikali hizo zinakusanya kati
ya asilimia 10 na 12 pekee.
Hii programu ni nini?
Serikali
kwa kipindi cha kuanzia mwishoni mwa miaka ya 1990 imekuwa ikitekeleza
kwa awamu Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma (Public
Finance Management Reform Progamme – PFMRP).
Lengo la programu hii bu kudhibiti na kujenga nidhamu ya fedha za umma katika Serikali na taasisi zake.
Mafanikio
yamepatikana katika maeneo ya kuongeza makusanyo ya mapato ya ndani,
udhibiti wa madeni, kutumika kwa mipango ya muda wa kati; usimamizi wa
misaada na fedha za washirika wa kimaendeleo, uwazi katika kutathmini
matumizi ya umma, mapitio ya sheria na miongozo ya usimamizi wa fedha,
ununuzi na ugavi wa rasilimali za umma.
Awamu ya kwanza hadi ya tatu
Awamu
ya kwanza ya programu hii ya kuanzia mwaka 1998 hadi 2004 ililenga
kudhibiti matumizi ya Serikali, kuhakikisha kuwepo kwa nidhamu ya mapato
na matumizi ya Serikali na kuchangia katika kukuza uchumi endelevu
Awamu
ya Pili iliyoanza mwaka 2004 hadi 2008 ililenga kuboresha taratibu na
mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kwa kutumia viwango vya kimataifa
ikiwa ni pamoja na kuhakikisha rasilimali zinatengwa kimkakati katika
maeneo ya vipaumbele.
Awamu
ya Tatu iliyojiri kati ya mwaka 2008 na 2012 ilikuwa ilijielekeza
katika kuhakikisha kuwa, mbinu na mifumo iliyowekwa katika awamu ya
kwanza na ya pili inaoanishwa na kutumika ipasavyo ili kuleta matokeo
yaliyokusudiwa
Usimamiaji Fedha Awamu ya Nne
Programu ya Maboresho ya Usimamizi wa Fedha za Umma Awamu ya Nne ndio tunayoendelea nayo hadio sasa. Utekelezwaji wake ni kuanzia kipindi cha mwaka wa fedha 2012/13 hadi 2016/17.
Lengo la awamu ni kuhakikisha kunakuwa na nidhamu katika Usimamizi wa Fedha za Umma na kutoa huduma bora kwa Umma ili kuleta Maendeleo Endelevu
Maeneo ya kuboresha
Eneo
la Kwanza la kuboresha ni usimamizi wa Mapato. Eneo hili linahusu
kuboresha makadirio na ukusanyaji wa mapato na kuhuisha Sera, Sheria na
Kanuni za Mapato.
Matokeo
yanayotarajiwa ni kuimarisha mifuo, michakato na taratibu kwa ajili ya
kuboresha uweza wa utendaji wa ukusanyaji wa mapato.
Eneo
la pili ni Mpango na Bajeti ambapo linalenga kuboresha sera za fedha,
mipango, bajeti ya muda wa kati na kuanzishwa kwa mpango na bajeti ya
kiprogramu (programme based budgeting).
Eneo hili litazingatia pia uboreshwaji wa takwimu za kibajeti (GFS Codes 2001) na uchambuzi wa shughuli za Serikali (CoFoG).
Matokeo
yanayotarajiwa ni kuimarisha uwezo wa kupanga na usimamizi wa bajeti,
ikiwa ni pamoja na matokeo na bajeti za kipgoramu ndani ya Wizara ya
Fedha, idara zinazojitegemea, Wakala za Serikali na Serikali za Mitaa.
Eneo la tatu ni la utekelezaji wa bajeti, uwazi na
uwajibikaji.
Eneo
hili linalenga kuhakikisha uhalisi wa maoteo ya bajeti ya matumizi,
kuboresha uwezo wa ununuzi, usimamizi wa fedha na madeni na kupanua
wigo, utunzaji na utoaji bora wa taarifa za fedha.
Matokeo yanayotarajiwa ni kuboresha matumizi ya rasilimali za umma kwa njia bora zaidi, ufanisi na uwazi.
Eneo
la nne ni usimamizi na udhibiti wa bajeti. Eneo hili linahusisha kutoa
miongozo ya kiutaalamu na kujenga uwezo kwa wizara na idara
zinazojitegemea sambamba na Wakala wa Serikali, Sekretariati za mikoa na
Serikali za Mitaa katika maeneo ya ukaguzi wa ndani.
Matokeo
yanayotarajiwa ni Kuboresha Usimamizi na utekelezaji wa udhibiti wa
ndani wa fedha, kanuni, sheria, taratibu na mapendekezo ya ukaguzi
katika Wizara, idara zinazojitegemea, Wakala wa serikali, Sekretariati
za mikoa na Serikali za Mitaa.
Eneo la tano linajielekeza katika usimamizi wa mabadiliko, ufuatiliaji wa program na nawasiliano.
Eneo
hili linahusika na masuala mtambuka katika maeneo ya mabadiliko ya
menejimenti, uongozi, uratibu, ufuatiliaji, mawasiliano kwa wadau wote
na muingiliano wa mifumo ya fedha ambayo ni muhimu kwa utekelezaji wa
program.
Matokeo
yanayotarajiwa ni kuboresha usimamizi na kuongeza uwajibikaji katika
uongozi ili kusimamia vizuri utekelezaji wa program.
Usimamizi wa programu awamu ya nne utafanyika kupitia yafutayo:
Mosi
ni kamati ya pamoja (Joint Steering Committee) ambayo itatoa mwongozo
wa kimkakati, kupitia na kuidhinisha Mpango na Bajeti na Mpango kazi, na
kufuatilia utekezaji wa programu.
Pili,
Kamati ya Utendaji ya Programu ambayo inawajibika katika kuchambua
mipango na bajeti, taarifa za utekelezaji zilizoandaliwa, kupitiwa na
kukubaliwa na Jopo la Utandaji la Watalamu kabla ya kuwasiliashwa kwenye
Kamati ya Pamoja.
Tatu
ni Japo la Utendaji la Watalaamu ina maamuzi juu ya masuala ya kitaalam
na kutoa mapendekezo kwa Kamati ya Utekelezaji ya Programy na mapitio
ya utekelezaji wa programu
Mafanikio ya programu
Baadhi
ya mafanikio ya programu yaliyopatikana katika awamu zilizopita pamoja
na kuanishwa kwa Sheria ya Ukaguzi wa Umma Namba 11 ya mwaka 2008 ambayo
imeimarisha kazi ya ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Sheria
hii imemuongezea uhuru Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali
(CAG), kufanya ukaguzi kwa ufanisi zaidi na hivyo kuongeza uwazi na
uwajibikaji.
Pili
ni marekebisho ya Sheria ya Fedha za Umma ya mwaka 2001 yaliyofanyika
mwaka 2010. haya yaliwezesha kuanzishwa kwa Idara ya Mkaguzi Mkuu wa
Ndani wa Serikali. Marekebisho hayo pia yalimpa mamlaka Mlipaji Mkuu wa
Serikali na Mhasibu Mkuu wa Serikali kusimamia na kufuatilia fedha za
Mamlaka za Serikali, hivyo yameruhusu kufanya malipo ya Serikali kwa
mtandao (Electronic Funds Transfer).
Mafanikio
mengine ni Mtandao wa malipo wa Serikali (IFMS) ulioanzishwa kwa ajili
ya kusaidia kuthibiti Matumizi ya fedha za umma na kusaidia kuandaa
taarifa za fedha.
Nne, taasisi za umma zimejengewa uwezo wa kufanya ununuzi kwa kuzingatia Sheria ya Ununuzi wa umma ya mwaka 2004.
Tano,
mpango Mkakati wa Muda wa Kati, Mwongozo wa Bajeti na mfumo wa
maandalizi wa matokeo ya bajeti na mgawanyo wa rasilimali katika maeneo
yenye vipaumbele (SBAS) vilianzishwa.
Sita, takwimu za kibajeti za Serikali (GFS code) ziliboreshwa kutoka GFS 1986 kwenda GFS 2001.
Saba,
Mfumo wa Ulipaji wa Mishara za Watumishi wa Serikali umeunganishwa
katika mikoa yote na hivyo kurahisisha uingizwaji wa kumbukumbu za
watumishi katika kila kituo.
Nane,
programu hii imewezesha Mkakati wa pamoja wa Misaada kwa Tanzania
kuanzishwa ili kuongoza taratibu za misaada na muundo wa mijadala.
Manufaa
mengine ya programu hii ni kuanzishwa kwa mfumo wa utoaji wa taarifa za
misaada na mikopo ya kigeni ili kuwezesha usimamizi na ufuatiliaji.
Changamoto
Si
rahisi kuanzisha programu kama hii na kisha kukoeskana kwa ka
changmoto. Moja ya changamoto hizo ni kuboresha mapato na Maoteo ya
mtiririko wa fedha za serikali kulingana na bajeti ili kutekeleza
vipaumbele.
Pili
ni kuimarisha utendaji wa mifumo ya usimamizi wa fedha za umma katika
ngazi ya Serikali za Mitaa. Tatu, ni linganifu na mahusiano ya mifumo
(harmonization of Systems).
No comments:
Post a Comment