Mkurugenzi wa
Uendelezaji Biashara wa NHC, David Shambwe akizungumza wakati wa hafla
ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Shirika la Nyumba la Taifa
(NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL), leo mchana,
makubaliano hayo yataziwezesha pande hizo mbili kushirikiana kibiashara
ambapo USL itapewa kipaumbele kwenye kupanga katika miradi ya ujenzi ya
majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa popote nchini.
Meneja
Mkuu wa Uchumi Supermarkets Tanzania, Chriss Lenana akifafanua Jambo
kwenye tukio hilo la utiani saini makubaliano baina ya pande hizo mbili,
lililofanyika kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo.
Viongozi
wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania
Limited (USL) wakisikiliza kwa kina maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwenye
mkutano huo
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano akizungumza kwenye tukio
hilo la utiani saini makubaliano baina ya pande hizo mbili,
lililofanyika kwenye hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam leo mchana.
Baadhi ya watendaji wa Uchumi na NHC wakifuatilia jambo kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya watendaji wa NHC wakifuatilia jambo kwenye hafla hiyo.
Viongozi
wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania
Limited (USL) wakisikiliza kwa kina maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwenye
mkutano huo
Viongozi
wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania
Limited (USL) wakisikiliza kwa kina maelezo yaliyokuwa yakitolewa kwenye
mkutano huo
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo mchana huu.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo mchana huu.
Baadhi
ya watendaji wa NHC wakifuatilia jambo kwenye hafla hiyo, Kushoto ni
Susan Omari, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC,
Muungano Saguya, Meneja Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC,
Mkurugenzi wa Uendelezaji Biashara wa NHC, David Shambwe, Meneja Mauzo
wa NHC, Tuntufye Mwambusi na Meneja Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu, Bulla
Boma.
Viongozi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL) wakiwa katika picha ya pamoja.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu katika
picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
Watendaji Uchumi
Supermarkets Tanzania Limited (USL) na Shirika la Nyumba la Taifa
wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa (NHC) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano.
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu akiwa
katika picha ya pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan
Ciano na watendaji wake.
Viongozi
wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania
Limited (USL) wakikata keki kuashiria kuanza kwa ushirikiano endelevu
baina ya NHC na USL
Mkurugenzi
Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Nehemia Kyando Mchechu
akitiliana saini hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi,
Dk. Jonathan Ciano.

wakibadilishana hati ya makubaliano na Afisa Mtendaji Mkuu wa Uchumi,
Dk. Jonathan Ciano
.....................................................................................
SHIRIKA
la Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL),
leo mchana wametiliana saini makubaliano yatakaziwezesha pande hizo
mbili kushirikiana kibiashara ambapo USL itapewa kipaumbele kwenye
kupanga katika miradi ya ujenzi ya majengo ya Shirika la Nyumba la Taifa
popote nchini.
Akizungumza
wakati wa hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Shirika la
Nyumba la Taifa (NHC) na Uchumi Supermarkets Tanzania Limited (USL),
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba alisema makubaliano hayo
yataziwezesha pande hizo mbili kufaidika na makubaliano hayo.
“Tunachkishuhudia
hapa Serena leo ni makubaliano kati ya pande mbili hizi yatakayowezesha
kukuza biashara nchini na hivyo kuwafanya Watanzania wengi zaidi
kuimarika kiuchumi kwani NHC itafungua fursa kwa uchumi na Uchumi pia
watafungua fursa kwa NHC. Miaka ya nyuma kidogo nilipokwenda Kenya
nilivutiwa na namna ambavyo Uchumi wanakuza uchumi wa Kenya kwa kununua
bidhaa za wakulima wa Kenya, natarajia kile kilichofanyika kule
kitafanyika hapa Tanzania pia, kwani ukuaji wa biashara na pesa hauna
mipaka,”alisema.
Alisema
kwa Uchumi imeweza kutumia fursa hiyo itakayoiwezesha kupata kipaumbele
kwenye miradi ya majengo ya biashara popote pale Tanzania na akatoa
wito kwa taasisi, mashirika na vyombo vingine kutumia fursa hiyo ili
uchumi wan chi uweze kukua.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Uchumi, Dk. Jonathan Ciano alisema kuwa Kampuni yake
imefurahishwa kuingia katika makubaliano hayo ambayo yataiwesha sasa
kupata maeneo bora ya kufanyia biashara kwani wameweza kuingia
makubaliano na mwendelezaji nambari moja wa miliki ambaye ataweza kuwapa
maeneo mazuri kwajili ya uwekezaji kibiashara.
Alisema
watayaenzi makubaliano hayo na hivyo kumudu kukuza uchumi wa
Watanzania kwa kuweza kununua bidhaa zao na kuziuza kwenye Supermarkets
zao.
Hafla
hiyo ilihudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwamo watendaji wa Mamlaka ya
ukuzani mitaji na masoko nchini na wadau wengine mbalimbali.
No comments:
Post a Comment