Afisa
Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Gaudensia
Simwanza(kushoto) akiwaeleza waandishi wa kuhusu udhibiti wa vyakula
vilivyoongezwa virutubisho wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi
wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es salaam. Kulia ni
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari Bi. Zamaradi Kawawa.
Na Frank Mvungi
Serikali
imejipanga kufanikisha mpango wa Kitaifa wa urutubishaji vyakula na
kusimamia usalama wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi kwa lengo la
kulinda afya ya walaji.
Hayo
yamesemwa na Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA)
bi Gaudensia Simwanza wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo
jijini Dar es salaam.
Akifafanua
Gaudensia amesema TFDA imeandaa kanuni za uongezaji virutubishi kwenye
vyakula (Tanzania food, Drugs and Cosmetics (food fortification)
Regulations 2012)
Alisema
kuwa hatua nyingine ni kuandaa miongozo ya udhibiti wa ubora na usalama
wa vyakula vilivyoongezwa virutubishi ili kuwajengea uwezo wasindikaji
kuweza kutekeleza matakwa ya kanuni za uongezaji virutubishi kwenye
vyakula.
Akifafanua Gaudensia
alisema kuwa upo mwongozo wa uhakiki wa ubora na usalama katika
usindikaji wa mafuta ya kula yaliyoongezwa virutubishi na mwongozo wa
uhakiki wa ubora na usalama katika usindikaji wa unga wa mahindi
ulioongezwa virutubishi ili kuliunda afya ya mlaji.
Katika
hatua nyingine Gaudensia alibainisha kuwa mwongozo wa usimamizi wa
Kanuni za uongezaji virutubishi na mwongozo wa ukaguzi wa vyakula
vilivyoongezwa virutubishi ambapo pamoja na mambo mengine mwongozo huu
umeainisha taratibu za kufuata katika udhibiti wa vyakula vilivyoongezwa
virutubishi muhimu katika chakula.
Vilevile alisisitiza
kuwa utoaji wa mafunzo kwa wadau kuhusu uhakiki na udhibiti wa ubora na
usalama wa vyakula vilivyooongezwa virutubishi kama vile wataalamu
kutoka katika viwanda ni muhimu kwa vile vinavyoongeza virutubishi
kwenye vyakula.
Katika
hatua nyingine, jukumu jinguine la TFDA ni kusambaza vitendea kazi
vinavyotumika katika uhakiki na udhibiti wa ubora na usalama wa vyakula
na kusimamia utekelezaji wa kanuni za uongezaji wa virutubisho kwenye
vyakula.
Aidha,
Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inafanya majaribio
katika Halmashauri 6 za Mikoa ya Iringa, Kilolo, Iringa Vijijini,
Njombe, Arusha, Karatu, Meru na Monduli ambapo kwa upande wa mafuta ya
kula majaribio yanafanyika katika Mikoa ya Manyara, Singida na Dodoma.
|
ILA NYIE CCM NI NOMA SANA, YAANI UBAYA UBWELA
-
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
NILIKUWA Najiongelesha tu kichwani kuhusu hii CCM basi nikajikuta nacheka
tu,ndio kununa siwezi. CCM kwa jinsi walivyo hawa ...
5 hours ago
No comments:
Post a Comment