|
Ili nchi yetu iondokane na aibu inayosababishwa na wachache
ni sharti sasa wananchi tukubali kuishauri serikali iwekeze katika ujenzi wa
KITUO CHA TAIFA CHA MICHEZO. Kituo ambacho kitanufaisha vipaji vya michezo yote
bila kubagua, kituo ambacho kitakuwa ‘Kiwanda cha Kuibua Vipaji vya kuiletea
nchi sifa. |
|
Tangu
mwaka 2006 wadau tulifanya juhudi za kupeleka mipango yetu serikalini
ili wahusika wa maswala ya michezo wapate kushauriana nasi jinsi ya
kutatua tatizo sugu ambalo linaikumba nchi yetu. Mifano ya (ramani na
picha) hizo zilikuwa zikitupiwa kapuni ili "Bwana Mkubwa" asione. |
|
'Hatimaye
mapema mwaka huu idea zetu hizi zilifika kwa wahusika wa juu kabisa na
hatua za IMPLEMENTATION zimeanza kwa amani na uzalendo usiokuwa na
kipimo'
Wadau
wazalendo tunaomba mawazo na ushauri zaidi ili mwisho wa siku Tanzania
yetu ifikie hatua ya kutabasamu pindi timu zetu zinaporejea nyumbani
kutoka kwenye viwanja vikubwa vya dunia. CHANZO : Gidabuday Blog
No comments:
Post a Comment