Watoto wea kijiji cha Mlangali wakifurahi kushika mwenge wa Uhuru |
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachel Kassanda akimpongeza mwanamke mwenye ulemavu wa macho Bi Regina Kayombo kwa ujenzi wa nyumba ya kisasa |
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru taifa Rachel Kassanda akionya utumiaji wa madawa ya kulevya huku mmoja kati ya askari akichochea bangi iliyoteketezwa na kiongozi huyo wilayani Ludewa |
Mwananchi wa Ludewa mjini akishiriki kukimbiza Mwenge baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya lami mjini Ludewa |
Vijana wakimbiza mwenge kitaifa wakiondoka eneo la Manda leo asubuhi |
kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa Rachel Kassanda wa tatu kulia akiruka kwa ukakamavu na askari wengine wakati wa mbio hizo wilayani Ludewa |
.............................. .............................. .............................. ..........................
Na Francis Godwin Blog -Ludewa
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa
Rachel Kassanda amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo
Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali za kimaendeleozinazofanyika
katika jimbo hilo na huku akimshambulia diwani wa kata la Mlangali
Faraja Mlelwa (Chadema) kwa kushindwa kushiriki mbio za mwenge katika
kata yake.
Alisema
kuwa miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya Tsh bilioni 3 ambayo mwenge
wa Uhuru mwaka 2014 unaipitia katika jimbo la Ludewa na wilaya ya
Ludewa kuwa ni miradi mikubwa ambavyo ni wazi mbunge wa jimbo hilo
Filikunjombe amefanya kazi kubwa hasa ukilinganisha na majimbo mengine
ambayo miradi yake haifikii thamani hiyo .
Kiongozi huyo alitoa pongezi hizo leo wakati wa kuzindua nyumba ya bora ya mkazi wa Mlangali Ndani Khamis Ignas Kayombo .
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Rachel Kassanda akimpongeza mbunge wa jimbo la LudewaDeo Filikunjombe kwa kanzi nzuri ya kuwaletea wana Ludewa maendeleo |
Alisema kuwa mbio za mwenge wa Uhuru zimekuwa zikihamasisha maendeleo katika
maeneo mbali mbali na viongozi wapenda maendeleo wakiwemo wabunge
na madiwani hawana budi kushiriki mbio hizo
kama ambavyo wananchi wana wamekuwa wakifanya .
Kwani
alisema hata kama diwani huyo alikuwa na majukumu yake binafsi
hakupaswa kuwakimbia wananchi wake ambao wamejitokeza
kuupokea mwenge na kuwa kitendo cha diwani kushindwa kushiriki
ni wazi kuwa ni diwani asiyependa maendeleo katika eneo lake.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kulia akimtazama mwandishi wa TBC Bw Msigwa wakati akiendelea kukusanya habari za mwenge |
“Ndugu zangu watanzania na wananchi wa
Mlangali wilaya ya Ludewa kwanza napenda kumpongeza mbunge wenu Deo
Filikunjombe natambua jitihada mbali mbali za kimaendeleo ambazo amekuwa
akizifanya ndani ya jimbo la Ludewa na nje ya jimbo kwa maana ya
mchango wake mkubwa katika bunge la jamhuri ya muungano wa
Tanzania ila ninapenda kuwaeleza wazi kuwa ni viongozi wachahe
wa kisiasa ambao wamekuwa wakiacha posho bungeni na kushiriki mbio za
mwenge kama ilivyo kwa Filikunjombe ninampongeza sana ila kama
kiongozi wa mbio za mwenge sijapendezwa na kitendo cha diwani wenu
kushindwa kufika hapa leo “
Hata hivyo
alisema wananchi hawana sababu ya kuendelea kuwasikiliza
viongozi wa vyama vya siasa ambao wamekuwa wakipinga mbio za mwenge
kwani mwenge wa Uhuru si mwenge wa chama cha siasa ila upo kwa ajili
ya watanzania wote na ni sehemu ya kudumisha mshikamano wetu na
kuenzi amani yake pamoja na kuhamasisha maendeleo miongoni mwetu.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Kassanda akiwa na Bw Khanmis Kayombo na mkewe baada ya kuzindua nyumba yao ene la Mlangali Ndani |
Hivyo
kiongozi yeyote wa kisiasa ni lazima kuendelea kuenzi mshikamano wetu
na kushiriki katika mbio hizo ambazo zilihasisiwa na baba wa Taifa
hayati Julius Nyerere ambae kwa sasa kanisa la RC limepata kumtangaza
kuwa miongoni mwa watakatifu kutokana na mchango wake mkubwa
wa kuliletea taifa hili uhuru wake.
Pia alisema
kuwa wapinzani wanaosema Mwenge wa Uhuru umepitwa na wakati
na wakiingia madarakani watauweka katika jumba la makumbusho hawana nia
njema na nchi hii na kuwataka watanzania kuwapuuza watu hao na
ikibidi watu hao kwenda kumwomba radhi mjane wa baba wa Taifa
Maria Nyerere ambae kitendo cha wao kuusemea vibaya mwenge huo ni
sawa na kumtukana baba wa Taifa.
Picha na Francis Godwin Blog
Picha na Francis Godwin Blog
No comments:
Post a Comment