Mkurugenzi
Mtendaji wa Harvard Club Of Washington, Bi. Caren A. Pauley
akiutambulisha umoja wa wanafunzi waliowahi soma Chuo Kikuu cha Harvard
waishio Washinton Metro Area kwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani,
Mhe. Liberata Mulamula siku ya Jumatano July 2, 2014 umoja huo
ulipotembelea Ubalozi wa Tanzania kwa ajili ya kukutana na jumuiya
mbalimbali za Kitanzania na Taasisi zinazoshughulika na maswala ya
Tanzania na kuweza kuongea pamoja kufahamiana na kubadilishana mawazo.
Afisa
Immaculata Diyamett anayeshughulikia maswala ya Utalii kwenye Ubalozi wa
Tanzania nchini Marekani, akiwakaribisha wageni wote Tanzania House na
kuwaambia wajisikie wapo nyumbani.
Rais
wa Umoja wa Wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu cha Harvard (Harvard Club Of
Washington, Bi Yi-Fun Hsueh ambaye pia ni mmoja ya waratibu akiongea
machache na kumshukuru Balozi Liberata Mulamula kwa kukubali
kuwakaribisha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kuja kukutana na
Jumuiya za Kitanzania na taasisi mbalimbali kwa ajili ya kujuana na
kubadilishana mawazo.
Balozi
wa Tanzania nchini Marekanai Mhe. Liberata Mulamula akiwakaribisha
Umoja wa wanafunzi waliosoma Chuo Kikuu Cha Harvard waishio Washinton
Metro Area kikundi kinachobeba jina la Harvard Club of Washington
kwenye Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani na kuwaelezea kuhusu Tanzania
na vivutio vyake chini ni maelezo aliyokuwa akitoa Mhe.
Mhe. Balozi Liberata Mulamula akipokea zawadi toka kwa Rais wa Umoja huo Bi. Yi- Fun Hsueh.
Kwa picha zaidi bofya HAPA
No comments:
Post a Comment