Mkurugenzi
Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando (wa pili kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua rasmi Tamasha la
Filamu la nchi za Majahazi la 17 maarufu kama Zanzibar International
Film Festival (ZIFF). Kulia Msaidizi wa Kitengo cha habari ZIFF, Lara
Prieston, Kushoto ni Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi (Dean),
Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa "Has T" (wa pili kushoto) na
Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala (katikati).
--------------------------------------------------------------------
Na Andrew Chale
DUNIA inatarajia kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria ndani ya
viunga vya Ngome Kongwe ndani Mji Mkongwe wa Stone Town, Unguja, kwa
watu wa mataifa yote watakapoungana na kushuhudia ‘Hatma ya Pamoja’ (A
common Destiny) Juni 14 hadi 22, 2014, katika Tamasha la Kimataifa la
filamu la Zanzibar (ZIFF).
Tamasha
hilo maarufu kama filamu la nchi za Majahazi ZIFF, kwa mwaka huu
linatarajiwa kufanyika kwa mara ya 17, tokea kuanzishwa kwake.
Akizungumza
mapema leo jijini Dar es Salaam, kwenye halfa maalum ya uzinduzi wa
tamasha hilo la 17, kwa wandishi wa habari iliyofanyika Goethe Institut
kituo cha utamaduni, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Profesa Martin
Mhando, alisema tamasha hilo msimu wa mwaka huu linatarajiwa kuwa moto
kwani linakuja na mambo mbalimbali yenye kuleta mabadiliko ya hali ya
juu.
Ni
kutokana na mabadiliko hayo, Profesa Mhando anasema tasnia ya filamu
kwa Tanzania inahitaji kubadilika ikiwemo wasanii wenyewe kujituma na
hata kuingia darasani ili kufanya kazi zenye uhakika.
Akimaanisha
kila msanii wa filamu aweze kufikia malengo yake, hana budi kujifunza
na kushirikisha wale waliotangulia katika tasnia hiyo.
Anazungumziaje kaulimbiu ya ‘A Common Destiny’
Prof. Mhando amesema kauli mbiu ya mwaka huu yenye kusema Hatma ya
pamoja yenye maana ya ‘A common Destiny’, ina lengo la kuwakutanisha
watu wa mataifa mbalimbali kuwa kitu kimoja na kufurahia kwa pamoja
ikiwemo kubadilishana mawazo kwa pamoja kwa tasnia ya filamu, muziki,
kwa mlengo ya kujenga.
“Tukiwa na haja moja, kuishi kwa amani na kuleta mapinduzi ya kiuchumi,
kifikira na maendeleo kwa amani, ZIFF kwa kutumia dira hiyo hasa
kupitia filamu zetu za ndani zenye mchanganyiko wa utamaduni na asili
yetu.
“Wazanzibari
na hata wageni watakaoshuhudia filamu hizi wataweza kuchukua utamaduni
huo na kuupeleka nje kwa furaha kubwa katika kufikia hatma ya pamoja”
amesema Prof. Mhando.
Music
Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akisisitiza jambo wakati wa mkutano
na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na wasanii watakaotoa
burudani kwenye tamasha hilo.
Lupita Nyong’o, Genevieve ndani ya nyumba
Tukio
kubwa ambalo kwa sasa Tanzania hasa kwenye viunga vya Zanzibar na
nchi nyingine duniani katika tamasha hilo la 17, ni ujio wa msanii wa
Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o, atakayeudhuria utoaji wa tuzo hizo za
ZIFF mwaka huu.
Lupita
ambaye ametwaa tuzo za Oscar na nyingine nyingi na kupelekea kutikisa
Hollywood kwa sasa ni miongoni mwa mastaa watakaokuwa kwenye tamasha
hilo huku akitarajiwa kuambatana na wazazi wake wote wawili pamoja na
wadogo zake.
Prof.
Mhando amesema tayari wazazi wote wawili wa Lupita akiwemo Dorothy na
Peter Anyang’ Nyong’o, watakuwapo kwa siku zote 10 kwenye tamasha hilo
huku Lupita mwenyewe akiahidi kuangalia uwezekano wa kuhudhuria japo
katika utoaji wa tuzo kama ratiba za shughuli zake hazita mbana.
Prof.
Mhando alisema Lupita ni zao la ZIFF na ndiyo iliyomfungulia mwanya wa
kujulikana na baadaye alienda kusoma zaidi masuala hayo ya filamu,
ambapo alishiriki ZIFF 2007 kama Volunteer.
Mara
nyingi staa huyo amekua akihudhuria matamasha na halfa mbalimbali za
utoaji wa tuzo na zawadi zingine huku akiwa ameambatana na wazazi wake
wote wawili.
Lupita mbali na tuzo hiyo ya Oscar, kupitia filamu ya ‘12 Years a
Slave’ pia filamu hiyo imempatia tuzo mbalimbali zikiwemo: tuzo ya
Steve McQueen kama mwigizaji mwenye mvuto, mwigizaji bora wa kike
aliyeshirikishwa, ‘Academy Award’, ‘Screen Actors’ Guild Award’, ‘NAACP
Image Award’, ‘Independent Spirit Award’, ‘Broadcast Film Critics
Association Award’, na nyingine nyingi.
Genevieve Nnaji.
Mbali
na Lupita, katika kuongeza utamu wa tamasha hilo, mastaa wengine nguli
wa Afrika kwa mwaka huu wanaotarajiwa kuwapo katika ushuhudiaji wa
utoaji wa tuzo hizo ni pamoja na muigizaji na mwanamitindo nyota wa
Nigeria, Genevieve Nnaji.
Wengine
ni Amr Waked (Misri), Faouzi Bensaidi (Morocco), Nadia Buari, Richard
Mote Damijo ‘RMD’, John Dumelo, Desmond Eliot na Florence Masebe.
Afisa
Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa
Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na Filamu
iliyopewa jina la "Women with Altitude" iliyoandaliwa na WFP ambapo
ndani yake imeshirikisha wanawake wa kitanzania watatu waliofanikiwa
kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro wakiwa wameambatana na wenzao nane
kutoka Nepal na kuzungumzia changamoto mbalimbali wakati wa kupata elimu
na maisha kwa ujumla itakayoonyeshwa kwenye tamasha hilo tarehe
17/6/2014 saa 19:15 jioni ukumbi wa Old Fort visiwani Zanzibar.
Filamu ya Mandela kufungua pazia
Jumla
ya filamu 79, kutoka mataifa mbalimbali zinatarajiwa kuonyeshwa huku
filamu iliyoingia kwenye tuzo za Oscar, ya Mandela: ‘A Long Walk to
Freedom’ ndiyo itakayofungua pazia kwenye tamasha hilo, Juni 14.
“Katika filamu hizo 79 za kimataifa zitaoneshwa ZIFF, nyingi zikiwa
zinatoka katika nchi za Kiafrika na filamu ya Mandela imepata bahati ya
kuwa ya ufunguzi”, amesema Profesa Mhando.
Pia Profesa Mhando amesema kuwa zitakuwepo filamu zinatoka katika nchi
35 zikiwemo filamu fupi 38, filamu ndefu za kuburudisha 24 na makala
17.
Meneja
wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi "Dean" akionyesha kitabu chenye
ratiba nzima ya tamasha hilo litakalorindima visiwani Zanzibar kuanzia
Juni 14 hadi 22 mwaka huu.
Burudani zitakazopamba
Kwa
upande wake, Edward Lusala anayeshughulikia muziki kwenye tamasha hilo
la 17, anasema kuwa, wamejiandaa kutoa burudani ya aina yake ambayo
itaacha historia kwa mwaka huu.
Lusala amesema jumla ya makundi 18 yanatarajiwa kutumbuiza. Huku kwa
wasanii gwiji wakiwemo pia Didier Awadi kutoka nchi ya Senegal na Habib
Koite (Mali) wanatarajiwa kuja kuishika Zanzibar na viunga vyake.
“Wasanii Koite na Didier ni miongoni mwa wasanii wakubwa sana na wenye
heshima kubwa hasa kwa muziki wao kwani wanapiga kimataifa hasa katika
matamasha makubwa na wamekuwa wakipiga miziki ya kipekee. Hivyo watu
wote watafurahia” amefafanua Lusala.
Ameongeza
kuwa, wasanii wengine ni pamoja na Farid Kubanda ‘Fid Q’, Ambwene
Yesaya ‘ Ay’, Sauti Soul, Mzungu Kichaa, Ras Inncent Nganyagwa, Grace
Matata na wengine wengi ambao watatoka Tanzania.
Na
kuongeza kuwa kwa sasa AY yupo nchini Malawi akijifua na moja bendi
maarufu ya muziki wa Live ambapo anatajiwa kukaa jukwaani kwa zaidi ya
lisaa limoja na nusu huku akiimbaLIVE.
Pia
vikundi vya muziki nguli toka Tanzania, Egypt, Kenya, Uganda, Malawi na
Afrika ya Kusini vitatumbuiza kila siku katika tamasha hilo.
Aidha, Lusala amesema kuwa, kwa mwaka huu wanatarajia kufanya
‘surprise’ kwa kumleta msanii mkubwa ambaye bado wapo kwenye mazungumzo
na msanii huyo kutoka Afrika kusini.
Kwa upande wake Meneja wa tamasha hilo, Daniel Nyalusi amewataja
wadhamini wa tamasha hilo ni pamoja mdhamini mkuu ZUKU Pay tv, huku
wengine ni Ethiopian Airlines, Tanzania Media Fund TMF, ComNet, Cello,
Air Uganda, Gina Din, FASTJET and United Petroleum. Wengine ni shirika
la Rosa Luzemburg Foundation, Arterial Networking, Steps International,
Azam marine, Prime Time Promotions, Goethe Institut na wengine wengi.
ZIFF
moja kati ya matamasha ya filamu makubwa duniani hukutanisha wadau
katika tasnia ya filamu. Wakiwemo waigizaji wa siku nyingi na maarufu,
waongozaji, waigizaji wachanga na wanafunzi kutoka ulimwenguni kote
Meneja
wa Biashara wa shirika la ndege la Fastjet, Jean Uku akizungumzia
udhamini wao kwenye tamasha hilo ambapo wametoa tiketi za safari ya
washiriki kutoka Afrika Kusini watakaoshiriki kwenye tamasha hilo.
Msanii
wa Hip Hop, Harry Kaale kutoka kundi la One "The Incredible" akielezea
namna watakavyotoa burudani na elimu kwa vijana kwenye tamasha hilo.
Msanii Mzungu Kichaa akiwashukuru ZIFF kwa kutoa nafasi kwa wazalendo kuonyesha vipaji vyao kwenye tamasha la ZIFF.
DJ maarufu Kahlil Jacobs-Fantauzzi kutoka Puerto rico akisisitiza kutoa burudani ya aina yake kwenye tamasha hilo. Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog
No comments:
Post a Comment