Viongozi
wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, wakipanda mti wakati
wa Uzinduzi wa Kampuni hiyo iliyoambatana na utoaji wa Msaada wa Vifaa
vya Michezo na vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya
pamoja na kutunza mazingra katika Shule ya Sekondari Miono na Kikaro
zilizopo Chalinze Mkoa wa Pwani.
Mwanafunzi
wa Shule ya Sekondari Kevin William na Alex Mode wa Shule ya Kikaro
wakichuana kuwania mpira baada ya kupokea msaada wa Vifaa vya Michezo na
vya mafunzo ya kuepuka matumizi ya madawa ya kulevya uliotolewa na
Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise.
Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Mwamtumu Mahiza kulia akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule
ya Sekondari Kikaro, Alex Mode, mbuzi aliyetolewa na Kampuni ya Bantu
Sports And Fitness Enterprise inayotoa elimu ya kupambana na mazingira
madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo pia kampuni hiyo imetoa vifaa
mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo. Miono Kikaro zilizopo
Chalinze Mkoa wa Pwani.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari, Kikaro wakiwa wamembeba juu juu Mbuzi waliopewa
na Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya
kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo baada ya
kuifunga timu ya Shule ya Sekondari Miono kampuni hiyo pia imetoa vifaa
mbalimbali vya michezo katika shule mbili hizo.
Mbia
wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya
kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo
Mashuleni, Said Said kulia akimkabidhi msaada wa vifaa vya kuelimisha
wanafunzi jinsi ya kuepukana na matumizi ya madawa ya kurevya Mwalimu wa
Shule ya Sekondari Miono, Ally Miango shuleni hapo juzi.
Mbia
wa Kampuni ya Bantu Sports And Fitness Enterprise, inayotoa elimu ya
kupambana na mazingira madawa ya kulevya na kuhamasisha michezo
Mashuleni, Adam Kasale, kushoto akimkabidhi msaada wa vifaa vya michezo
Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Kikaro, Gabriel Dominc baada ya Kampuni
hiyo kutoa msaada kwa shule hiyo na Miono zilizopo Chalinze Mkoa wa
Pwani, katikati ni Mkuu wa Mkoa huo, Mwamtum Mahiza.
No comments:
Post a Comment