MBUNGE AUAGA UKAPERA: MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI MHE. JOSHUA AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA BI. ANNA NNKO, USA RIVER JIJINI ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Sunday 8 June 2014

MBUNGE AUAGA UKAPERA: MBUNGE WA ARUMERU MASHARIKI MHE. JOSHUA AFUNGA PINGU ZA MAISHA NA BI. ANNA NNKO, USA RIVER JIJINI ARUSHA

"Mmetuona "ni kama ndio maneno yaliyokuwa vichwani mwao maharusi ,Joshua Nassari na Anande Nnko wakionesa vyeti vyao vya ndoa.
Gavana wa kwanza wa Tanzania Mzee Edwin Mtei na Mama Mtei pia walikuwa katika inada hiyo.
Wazazi wa Maharusi ,Joshua Nassari na Bi Anande Nnko.
Bw na Bi Joshua Nassari na wakiweka Sadaka zao katika kapu la sadaka.
Maharusi ,wakapata nafasi ya kusalimiana na Mzee Edwin Mtei.
Ibada ya ndoa ikawa imefika tamati na maharusi wakatoka kanisani tayari kwa msafara wa magari kuelekea uwanjani.
Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiwa mbele ya zawadi yao ya
Ng'ombe ilitolewa na waumini wa Kanisa la Kilinga ambako ibada ya ndoa
ilifanyika,kanisa linaloongozwa na Mchungaji Babu.

Mbunge Joshua Nassari na Anande Nnko wakiteta jambo .

Baba Mzazi wa Joshua Nassari,Mzee Samwel Nassari akimpongeza mwanae kwa hata hiyo.
Mamsapu akianza majukumu ya kuhakikisha Mzee anakuwa nadhifu kila wakati.
Maharusi wakaaga katika viwanja vya Kanisa la Kilenga .
Bi Harusi Anande Nnko akiwa katika gari tayari kuelekea katika viwanja vya Usa-River Academy.
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari na ,Anande Nnko
wakiwa ndani ya gari muda mfupi baada ya kufunga ndoa katika kanisa la
Kilinga wilayani Arumeru tayari kwa kuelekea viwanja vya  Usa-River
Academy.

Msafara ukaanza safari ya kuelekea barabara kuu ya Moshi/Arusha ukitokea kanisani Kilinga.
Baadae maharusi wakabadili gari ili waweze kuonekana vyema na wakazi wa jimbo la Arumeru Mashariki.
Maharusi wakiwa katika gari la wazi huku wakipunga mikono kwa watu waliokuwa barabarani.
Maharusi waki "Show Love"
Kila sehemu msafara wa magari ya maharusi ulipopita ,wakazi wa maeneo hayo walionesha furaha zao .
Barabarani kulijaa watu wakimshangilia Mbune wao akijinyakulia Jiko.
Kama kawaida Jasiri haachi asili na muacha asili ni hasidi na hana akili.
Msafara wa magari ulikuwa ni mrefu .

No comments:

Post a Comment