KATUNISTI WA TZ : MCHORA VIBONZO NATHAN MPANGALA AFANYA UTALII WA NDANI KILWA MASOKO - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Thursday, 5 June 2014

KATUNISTI WA TZ : MCHORA VIBONZO NATHAN MPANGALA AFANYA UTALII WA NDANI KILWA MASOKO

 Mnara wa kwa Bi. Adha, Kilwa Kivinje, Lindi. Kumbukumbu ya Wajerumani wawili waliuawa na wenyeji mwaka 1888 kwa imani kuwa walikwenda eneza dini ya Kikristo. Picha ndogo ni maelezo ya mnara huo.
 Mamlaka zinazohusika wamepasusa kabisaaaa...Hapa (Kilwa Kivinje, Lindi) ndipo walipolazwa Wajerumani waliodunguliwa katika vita ya Majimani, 1905 – 1907.
 Mchora vibonzo, Nathan Mpangala (kulia), akistaajabu gofu ya iliyokuwa Ngome ya Kilwa, lililopo Kilwa Kisiwani, Lindi. Kwa mujibu wa muongoza wageni Bw. Samuel, anasema mjengo huo ambao ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kulinda kisiwa, ulijengwa karne ya 16 na Wareno. Ilipofika karne ya 19 Waarabu wakaunakshi nakshi zaidi.
  Hili gofu laitwa Makutano Palace, limejaa tele Kilwa Kisiwani, Lindi. Moja ya kumbukumbu zake inadaiwa katika karne ya 18, Sultan wa Oman, Bw. Ibrahim alilitumia kuingia mkataba wa kumpa watumwa (babu zetu na bibi zetu), mfanyabiashara wa Kifaransa Bw. Moris. Uliopumzika ardhini ni mabaki ya mzinga uliotumika kusasambulia ‘maadui’. 
Mchora vibonzo, Nathan Mpangala akiwa mbele ya gofu la Makutano Palace lililo Kilwa Kisiwani, Lindi hivi karibuni. Hakika Tanzania ni zaidi ya tuijuavyo!
 Mchora vibonzo, Nathan Mpangala akiwa makaburi ya Familia ya Sultani wa Kilwa, Al Hassan Bin Suleiman, Kilwa Kisiwani, Lindi hivi karibuni. Makaburi haya yanayodaiwa ya karne ya 16 yana alama ambazo ni rahisi kugundua lipi la mwanaume na lipi la mwanamke.
Mchora katuni, Nathan Mpangala (mwenye sanigogozi) akisikiliza simulizi toka kwa wenyeji wa Kitongoji cha Masakasa Mpala, Kilwa Masoko, Lindi hivi karibuni. Mzee Hamis Sumri (aliyetinga kitu cha Arsenal) anasema, sifa moja ya kitongoji chao ni hii; kiliwatoa Salum Chanza, Ali Juma, Idd Hamis na Mzee Juma kwenda kushiriki vita ya pili ya dunia kati ya Mjerumani na Mwingereza na walirudi salama salimini.

No comments:

Post a Comment