Mkuu
wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi akiongea na wadau mbalimbali wa
elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za msingi na
sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa hafla ya Siku
ya Elimu mkoani Dar es salaam leo.Katika hafla hiyo washindi wa
mitihani ya taifa kwa mwaka 2013 kutoka shule za msingi na sekondari za
serikali na binafsi wametunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kutokana na
ufanisi wao katika utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Afisa
Elimu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Raymond Mapunda akiongea na wadau
mbalimbali wa elimu wa mkoa wa Dar es salaam wakiwemo walimu wa shule za
msingi na sekondari,wamiliki wa shule binafsi na wanafunzi wakati wa
hafla ya Siku ya Elimu mkoani Dar es salaam.
Baadhi
ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari za jijini Dar es salaam
waliohudhuria hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar Es Salaam wakifuatilia
matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea wakati wa hafla hiyo.
Wadau
wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi,
wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakishangilia mafanikio
na ushindi wa mkoa wa Dar es salaam katika mitihani ya taifa ya shule
za Msingi na Sekondari kwa mwaka 2013 leo jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya Siku ya Elimu.
Mkurugenzi
wa Shule ya shule ya Sekondari ya Tusiime ya jijini Dar es salaam Bw.
Albert Katagira akipokea cheti cha ushindi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Mhe. Raymond Mushi (kulia) kufuatia shule yake kutoa wanafunzi
bora katika ufaulu wa masomo katika mitihani ya taifa kwa ngazi ya taifa
na mkoa wa Dar es salaam kwa shule binafsi.
Mwalimu
Stella Kasheba (kulia) kutoka shule ya Sekondari Zanaki akipokea cheti
cha ushindi kwa niaba ya Mkuu wa shule hiyo kufuatia shule ya Sekondari
Zanaki ya jijini Dar es salaam kutoa mshindi Bora wa Jumla kwa shule za
sekondari za serikali katika mitihani ya taifa kwa mwaka 2013.
Mwanafunzi
Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akipokea cheti cha
pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla katika mitihani ya Taifa kwa
mwaka 2013 kwa shule za Binafsi za jiji la Dar es salaam.
Mwanafunzi Hussein Hemed Hussein wa Shule ya Msingi Tusiime akionesha cheti
cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla kwa wavulana katika mitihani
ya Taifa kwa mwaka 2013 kwa shule za Binafsi za jiji la Dar es salaam
alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi katika
hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar es salaam.
Mwanafunzi Joyce Lymo wa Shule ya Sekondari Kanosa, Kinondoni akionesha cheti
cha pongezi kwa kuwa mshindi Bora wa jumla kwa wasichana katika
mitihani ya Taifa kwa mwaka 2013 alichokabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya
Ilala Bw. Raymond Mushi katika hafla ya Siku ya Elimu jijini Dar es
salaam.
Wadau
wa elimu wakiwemo wazazi, walimu wa shule za sekondari na msingi,
wamiliki wa shule binafsi na viongozi mbalimbali wakifuatilia matukio
mbalimbali wakati wa hafla ya Siku ya Elimu mkoa wa Dar es salaam.
Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.
No comments:
Post a Comment