Mwigizaji
na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity,
Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kushoto) akizungumza na waandishi wa
habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam juzi baada ya kuteuliwa
kuwa msimamizi wa mkuu Wasanii wa nje ya Bunge Maalum, kulia ni Makamu
Mwenyekiti wa Tanzania Kwanza nje ya bunge, Renatus Muadhi, na katikati
ni Mwenyekiti wa Taasisis hiyo, Agustino Matefu.
Mwigizaji
na Mchekeshaji ambaye ni Mwenyekiti wa Kundi la Bongo Movie Unity,
Steven Mengere 'Steve Nyerere' (kushoto) akikabidhiwa mkataba wa kuwa
msimamizi wa mkuu wa wasanii wa nje ya Bunge Maalum na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Tanzania Kwanza nje ya bunge, Agustino Matefu. Makabidhiano
hayo yalifanyika juzi jijini Dar es Salaam.
---
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
WASANII
wa Bongo Movie, muziki wa dansi, taarab, maigizo na tamthilia
wametangaza kuzunguka nchi nzima wakiwa na kamati ya Tanzania Kwanza Nje
ya Bunge Maalum la Katiba kwa lengo la kutangaza amani kwa vijana wa
rika lote bara na visiwani.
Baadhi
ya wasanaii hao ni pamoja na Steven Mengele ‘Steve Nyerere’ ambaye
ameteuliwa kuwa msimamizi mkuu wa uwakilishi kwa upande wa wasanii
katika Tanzania kwanza nje ya Bunge maalum, Muungano huo uko chini ya
Mwenyekiti Augustino Matefu.
Akizungumza
juzi na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Steve amesema kwamba
ataungana na wasanii ambao wako katika vyama mbalimbali kama vile Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo, NCCR, Mageuzi , Cuf na vyama vingine huku
wote wakiwa na lengo moja tu la kuhimiza mchakato wa katiba uendelee
huku wanasiasa wakizingatia kudumisha amnai na umoja wa Watanzania.
Nyerere
aliongeza kwa kusema kuwa yeye hakuwa na kipingamizi pindi alipoambiwa
amechaguliwa kuwa miongoni mwa wasimamizi wa mpango huo ambao
umewakutanisha vijana kutoka katika itikadi mbalimbali za vyama vya
siasa.
“Nilipoambiwa
hili jambo niliweka itikadi zangu za chama pembeni na kuuvaa Utanzania
kwanza ili kuunganisha fani zetu wote kwa pamoja na kuweza kuwahimiza
wananchi wadumishe amani tuliyokuwa nayo nchini” alisema Nyerere.
Aliongeza
pia kwa kuwaomba viongozi wa dini masheikh na maaskofu wakiwemo mapadri
wote kuungana nao wasanii hao katika kuhimizaani ya amani ya nchi.
“Sisi
wasanii tunapata riziki zetu kutokana na amani na utulivu uliopo nchini
mwetu hivyo kila msanii na Mmtanzania aone ni jambo la fedheha
kuiichezea amani ambapo siku ikipitea tutakwenda kuomba hifadhi katika
nchi za jirani zilizopata uhuru na kufuata ushauri kutoka kwetu”.,
Aliongeza
kwa kusema kwamba ana imani kubwa watanzania watawaelewa pindi
watakapokuwa katika ziara hiyo kuzunguka nchi nzima huku wakiwa na
mabalozi watano kutoka kila nyanja ya sanaa ambazo ni muziki wa taarab,
Hip Hop, Sanaa za maigizo, Michezo na tamthilia. Mkutano mkubwa
unatarajiwa kufanyika Kibanda Maiti Zanzibar.
No comments:
Post a Comment