Mtangazaji wa
kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa
Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali
ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji wa
kipindi cha Clouds FM, Dr Isaac Maro akikabidhi msaada wa vifaa kwa
Dr Muzdalifat Abeid, bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi hospitali
ya Temeke, ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji
wa Kipindi cha Power Breakfast, Paul James (PJ), akikabidhi msaada wa
pedi kwa mmoja wa wakina mama walio katika wodi ya wazazi wa hospitali
ya Temeke.
Msanii
wa mashairi na kughani, Mrisho Mpoto akikabidhi msaada wa pedi za
watoto kwa Mama Leah Othman katika hospitali ya Temeke ikiwa ni katika
kuadhimisha miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji wa Jahazi, Ephraim Kibonde akimfariji mmoja wa akina mama katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Temeke.
Mtangazaji
wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akimhoji mmoja wa vijana ambao
wameacha kutumia madawa kwa msaada wa kituo cha Keko Youth. Clouds FM
ilitembelea kituo hicho ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 na kutoa
msaada wa mashine ya kupaka rangi kwa vijana hao
Baadhi
ya wafanyakazi wa Clouds FM wakiwa katika picha ya pamoja na wanawake
waliokuwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Temeke, baada ya
kukabidhi misaada yao ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha miaka 14 ya Clouds
FM.
Mtangazaji
wa kipindi cha Ampilifaya, Millard Ayo akiwa amempakata mtoto, baada ya
kutembelea hospitali ya Temeke na kukabidhi misaada ikiwa ni sehemu ya
miaka 14 ya Clouds FM.
Mtangazaji wa
kipindi cha Club 10, Perfect Chrispin akikabidhi michango ya papo kwa
papo iliyotolewa na wafanyakazi wa Clouds FM kwa kituo cha mwanzilishi
wa kituo cha Keko Youth, Yohana Victor Haule. Mbele yao ni mashine ya
kupaka rangi iliyotolewa na Clouds FM kama msaada kwa kituo hicho.
Mwanzilishi wa
kituo cha Keko Youth, Yohana Haule akimkabidhi zawadi ya kuku Meneja wa
Vipindi wa Clouds, Seba Maganga, ikiwa ni kama shukrani kwa kutembelea
kituo chao.
========= ======= ========
Miaka 14 ya Clouds FM yaadhimishwa kwa shwangwe kubwa Shughuli za kijamii na burudani zatawala
Kituo cha Redio namba moja hapa nchini, Clouds FM kimefikia kilele cha mwezi wa maadhimisho ya miaka 14 toka kimeanzishwa. Maadhimisho hayo
ambayo yamefanyika kwa mwezi mzima sasa, yalianza na watangazaji wa
vipindi tofauti kwenda mikoa mbalimbali ili kuweza kusherekea miaka hii
14 pamoja na wasikilizaji wao sehemu walipo.
Ikiwa ndio siku ya kilele cha maadhimisho hayo, Clouds FM imetembelea
hospitali ya Temeke na kituo cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya kulevya cha Keko Youth, ambapo misaada mbalimbali imetolewa. Wakiwa katika hospital ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya hospitali katika wodi ya wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa vitendea kazi ambavyo vitawezesha vijana kujiajiri baada ya kumaliza matibabu.
hospitali ya Temeke na kituo cha kuhudumia vijana wanaotumia madawa ya kulevya cha Keko Youth, ambapo misaada mbalimbali imetolewa. Wakiwa katika hospital ya Temeke, Clouds FM imetoa vifaa mbalimbali vya hospitali katika wodi ya wanawake na watoto, huku Keko Youth wakipewa vitendea kazi ambavyo vitawezesha vijana kujiajiri baada ya kumaliza matibabu.
Akizungumzia maadhimisho
hayo ya Clouds FM, Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group, Joseph
Kusaga alisema sherehe hizi kwa mwaka huu ni za kipekee kwa Clouds FM
hasa kwa kuwa wameweza kufanikisha mambo mengi makubwa toka
walipoanza. ‘Maadhimisho haya ya miaka 14 kwa mwaka huu yana
lengo moja kubwa, kuwashukuru wasikilizaji wetu kwa kutufikisha hapa
tulipo, na ndio maana tumeanza kwa kuwapa misaada wanaohitaji, halafu
tunamalizia kwa burudani’’ alisema Kusaga.
Akielezea zaidi
mafanikio ya Clouds FM kwa kipindi cha miaka 14, Kusaga alisema redio
imefanikiwa kuwafikia watu wengi zaidi, imeongeza ubunifu lakini pia
kumekuwa na uboreshaji wa hali ya juu wa mitambo ya kutangazia pamoja
na maudhui.
‘Kwa kipindi
cha miaka mitatu mfululizo tumefanikiwa kushinda tuzo ya Super Brand,
na kwa mwaka huu pekee radio imefanikiwa kuanza kusikika mikoa
ya Njombe, Songea, Njombe, Sumbawanga, Katavi na Geita, kupitia mitandao
kwa wasikilizaji wetu nje ya nchi lakini pia tumefanikiwa kufanya
tamasha la Fiesta kwa mafanikio zaidi’ alisema Kusaga.
Kusaga pia
aligusia mchango wa Clouds FM katika kuhamasisha maendeleo na uzalendo
hapa nchini akitoa mfano wa semina za Fursa ambazo zilifanikiwa kwenda
nchi nzima zikizungumza na vijana kuamka na kuchangamkia fursa katika
sehemu wanazoishi. ‘Semina za Fursa zimekuwa mfano mkubwa namna
Clouds FM ilivoweza kutumia nguvu yake kama radio inayosikilizwa zaidi
katika kuchagiza maendeleo, na kwa hakika mafanikio ya semina yamekuwa
ni makubwa sana’ alisisitiza Kusaga.
Kusaga pia
alitoa shukrani za pekee kwa watanzania kwa kuinga mkono Clouds FM sio
kwa kusikiliza tu bali hata katika kuhudhuria matamasha na shughuli
nyingize za Clouds. Kilele cha maadhimisho ya miaka 14 ya
Clouds FM kitamalizika kwa burudani kubwa ambayo itafanyika katika
viwanja vya Mwembeyanga ambayo itajumuisha wasanii na watu wengine
maarufu.
‘Kumekuwa na
mafanikio makubwa katika redio yetu kwa kipindi cha miaka 14, na
naomba niseme, bila ninyi wasikilizaji wetu tusingeweza kufika hapa’
alimaliza Kusaga
No comments:
Post a Comment