NIKKI II Toka WEUSI/ARUSHA
Wengi
huanza kuchakaza viatu vyao wakipita ofisi moja baada ya nyingine
kuomba nafasi za kazi zilizotangazwa na mwishowe hujikuta wakiwa
wamefanya usaili zaidi ya ofisi 10 pasipo kuitwa kazini.
Kwa kawaida vijana wengi Afrika, hususan Tanzania wanapohitimu elimu ya juu, jambo ambalo hulifikiria ni kutafuta ajira.
Wengi
huanza kuchakaza viatu vyao wakipita ofisi moja baada ya nyingine
kuomba nafasi za kazi zilizotangazwa na mwishowe hujikuta wakiwa
wamefanya usaili zaidi ya ofisi 10 pasipo kuitwa kazini.
Hata hivyo hii ni tofauti na msanii wa
Hip
Hop kutoka Kundi la Weusi, Nickson Simon maarufu kama Nikki wa II
ambaye ana shahada ya Uzamili katika maendeleo kutoka Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam (UDMS).
Nikki
wa II ambaye pia ni mshindi wa tuzo za muziki za Kilimanjaro 2014 KTMA
kupitia wimbo Bora wa Hip Hop “Nje ya Box”, aliowashirikisha G Nako na
Joh Makini wote kutoka Kundi la Weusi, anasema licha ya kwamba amehitimu
elimu ya juu na kupata alama kubwa, hayupo tayari kuajiriwa.
Rapa
huyu ambaye ni mdogo wa damu wa mwanamuziki John Simon maarufu kama Joh
Makini wiki hii ameachia wimbo wake mpya “Sitaki Kazi” wimbo ambao
umebeba maudhui makubwa yenye kutoa elimu kwa vijana wa rika na elimu za
aina zote.
Msanii
huyu aliyeibukia katika fani mwaka 2008 na wimbo wake “Good Boy”
aliokuwa amemshirikisha Rama Dee, anasema hisia alizonazo ndizo
zilizomfanya atunge mistari ya wimbo huo, kutokana na maisha halisi ya
vijana wa sasa.
“Niliimba
wimbo huu kutokana na kuwaona vijana wengi wenye elimu ya juu
wakihangaika kupita huku na kule na vyeti vyao wakitafuta ajira, kwangu
mimi naona ni utumwa kwa msomi kutegemea kufanya kazi za watu wengine,
badala ya kuibua cha kwako ili utoe ajira kwa wengine,” anasema.
Hata
hivyo anabainisha kuwa namba ya vijana wanaohitimu stashahada, shahada
ya kwanza na kuendelea inazidi kuwa kubwa na ajira ni za kubahatisha.
“Ndani
ya mistari ya wimbo “Sitaki Kazi” kuna mistari inayoelezea namna kijana
anavyoweza kutatua tatizo la ajira kwa kubuni vitu mbalimbali ambavyo
vitazalisha pato na kuweza kuajiri maelfu ya vijana wanaohitimu mwaka
hadi mwaka,” anasema rapa huyo.
Anasema
ingawa nchi haina utaratibu maalumu wa kuwaandaa vijana pindi
watakapomaliza elimu zao, kuna haja ya kutafuta ufumbuzi wa tatizo hili
kwa vijana husika.
“Tatizo
kubwa katika nchi yetu hakuna mtu au utaratibu ambao unawaandaa vijana,
lakini sisi wenyewe lazima tutambue kwamba hii ni karne ya kutengeneza
ajira yetu wenyewe, ndiyo maana nimeimba wimbo huu ili kubadilisha
mtizamo na fikra za vijana ambao wanategemea ajira, ni lazima jamii
ibadilike,” alisema Nikki wa II.
Nikki
anasema katika usanii alionao anajivunia kufanya kazi hiyo kwani ni
kujiajiri inayomwingizia kipato kikubwa ukilinganisha na ajira ya
ofisini ambayo ingembana na asingeweza kupata fedha ya ziada nje ya
mshahara.
Anasema
hiyo inamfanya avutiwe na kazi yake kwani anaamini kwamba elimu
inamsaidia kuiboresha kazi yake, hivyo anaitumia kuongeza ujuzi katika
muziki na kazi mbalimbali za Kampuni ya Weusi.
“Kijana
lazima ujiamini kwamba unaweza kutengeneza ajira, watu ninaowapenda na
maarufu walifanya kazi katika jamii na kutoa ajira kwa vijana
wangakuwaje iwapo Biliget angeajiriwa, inakuwaje Bhakresa au Mohamed
Dewji wangeajiriwa? Leo hii maelfu ya Watanzania wasingekuwa na ajira,”
anasema.
Anasema
kiuna mambo mengi aliyoyazungumzia katika wimbo huo ikiwamo ubunifu kwa
kuwahamasisha vijana wawe wabunifu ili kukuza nafasi za ajira na
kuongeza pato la taifa.
“Sitafuti
kazi ila nataka nitafutwe na watu wanaotafuta kazi’, haya ni moja ya
mashairi yaliyopo katika wimbo huu ambao niliimba nikiwa na nia ya
kuwahamasisha vijana wawe wabunifu ili elimu tulizozipata tuweze
kuzitumia katika kukuza uchumi wa nchi na kujiendeleza sisi na familia
zetu,” anasema rapa huyo.
Nikki
wa II anatoa wito kwa vijana kujituma wao wenyewe kabla ya kufukuzwa
kazi, kwani wengi wao waliweza kufanya makubwa baada ya kufuzwa katika
kazi za kuajiriwa.
Anasema
ni vyema vijana wakajituma wao wenyewe kwa kufanya vile wanavyovipenda
kuliko kufanya kazi wasizozipenda kwa kutumikia mishahara.
“Wengi
wanafanya kazi wasizozipenda kwa kutumikia mishahara, mtu anafanya kazi
ili apate mshahara na hii inasababisha wengi kulipua kazi na wakati
mwingine kutotekeleza majukumu yao ya kikazi.”
“Iwapo
mtu atafanya kazi anayoipenda au kujiajiri hujikuta akifanya kazi mpaka
usiku wa manane na hapo tayari anakuwa ametengeneza pato kubwa kwake au
kampuni yake kwani anafanya kitu chenye masilahi kwake na siyo kwa
kampuni fulani au mtu binafsi,” anasema Nikki wa II.
Licha
ya kutoa darasa hilo kwa wasomi nchini, rapa huyo alirudi pia kwa watu
wa uswahilini na wale wasio na elimu na kuwataka kutokata tamaa na
kuishia kuomba ajira kwa watu wengine kwani na wao wana nafasi kubwa ya
kujituma na kumiliki makampuni makubwa.
“Mimi
nimezaliwa uswahini huko Arusha, ninavyojua mimi watu wengi wa huko
hawana CV wala vyeti, ndani ya wimbo huo kuna mistari nimeimba kwa ajili
yao,” anasema.
Kuhusu Nikki wa II
Kijana
huyu mzawa wa Daraja Mbili Arusha, alisoma Arusha Sekondari. Nikki
anafahamika zaidi kwa kazi zake kama Good Boy, Nje ya Box, Gere, Pea,
Kiujamaa, Bum Kubam na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment