Kwaya ikiimba wakati wa shughuli hizo.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe
(Mb.) amemtaja aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Marehemu
Flossie-Gomile Chidyaonga kama Malkia wa Amani kwa vile alikuwa mstari
wa mbele katika vikao vya usuluhishi na kutafuta amani kwenye Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) Malawi ikiwa ni
Mwenyekiti wa jumuiya hiyo.
Mhe.
Membe aliyasema hayo wakati wa mapokezi maalum ya Marehemu Balozi
Chidyaonga yaliyofanyika katika Uwanja wa Ndege wa Blantayre nchini
Malawi na kuhudhuriwa na Rais wa Malawi, Mhe. Joyce Banda, Viongozi wa
Serikali ya Malawi, Familia ya Marehemu, Taasisi za Dini, Mabalozi na
Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za mji huo.
Mhe.
Membe ambaye anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mhe. Jakaya Kikwete kwenye mazishi ya Marehemu Balozi Flossie
Gomile-Chidyaonga alisema kwamba Tanzania, Malawi, nchi za SADC na dunia
kwa ujumla imempoteza mwanadiplomasia mahiri ambaye aliujua na
kutekeleza wajibu wake ipasavyo.
“Kwa
niaba ya Mhe. Rais Kikwete, Watanzania wote na mimi binafsi nakuomba
Mhe. Rais Banda na Wananchi wa Malawi mpokee salamu zetu za pole kwa
kumpoteza Balozi Flossie ambaye alikuwa mstari wa mbele katika masuala
ya amani kwa Kanda ya SADC na ninamwita Malkia wa Amani kwa juhudi hizo
alisema Mhe. Membe”.
Mhe.
Membe aliongeza kusema kwamba kutokana na kufanya kazi kwa kujituma na
kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na Malawi, Marehemu Balozi
Flossie alikubalika Serikalini, kwa Mabalozi wenzake na hata katika
Taasisi za Elimu ya Juu kama Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako
alishiriki katika kutoa mihadhara mara kwa mara.
Katika
hotuba yake wakati wa mapokezi hayo, Rais wa Malawi Mhe. Joyce Banda
alisema kuwa wameupokea msiba huo wa ghafla kwa majonzi makubwa ambapo
kwa namna ya pekee aliishukuru Serikali ya Tanzania hususan Rais Kikwete
kwa ushirikiano wa hali ya juu aliouonesha tangu msiba utokee na kutuma
ujumbe mzito uliioongozwa na Waziri Membe kumsindikiza Marehemu Flossie
nchini Malawi.
“Mimi
binafsi na wananchi wa Malawi tunatoa shukrani za dhati kwa ndugu zetu
Watanzania hususan Mhe. Rais Kikwete kwa ushirikiano walioonesha katika
kipindi hiki kigumu kwetu. Mhe. Rais Kikwete aliwasiliana na mimi akiwa
safarini mara tu msiba ulipotokea. Alielezea kushtushwa na msiba huo wa
ghafla kama mimi nilivyoshtushwa. Nilimweleza azma ya Serikali yangu
kuhusu kutuma ndege kwa ajili ya kuufuata mwili wa ndugu yetu Flossie
lakini alisema nimwachie hilo ni jukumu lake na amelitekeleza
kikamilifu kama tunavyoona” alisema kwa masikitiko Mhe. Banda.
Awali
akizungumza kwa niaba ya Familia ya Marehemu Balozi Flossie, Msemaji wa
Familia hiyo Bw. Andrew naye aliishukuru Serikali ya Tanzania na
kusema kuwa ushirikiano uliooneshwa katika kipindi hiki kigumu kwao
unadhihirisha undugu mkubwa uliopo kati ya Tanzania na Malawi.
Baadhi
ya Viongozi wa Serikali na Mabalozi waliofuatana na Mhe. Mhe. Membe
kwenye msiba huu ni pamoja na Bw. John Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya
Mambo ya Nje na Ushirikano wa Kimataifa, Balozi Vincent Kibwana,
Mkurugenzi wa Idara ya Afrika, Kaimu Mkuu wa Mabalozi wanaowakilisha
nchi zao Tanzania ambaye pia ni Balozi wa Zimbabwe, Balozi wa Zambia
nchini, Mhe. Judith Kangoma, Balozi wa Norway nchini na Maafisa wa
Ubalozi wa Malawi nchini.
Marehemu
Balozi Flossie Gomile-Chidyaonga ambaye alifariki dunia katika
Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam tarehe 09 Mei, 2014
anatarajiwa kuzikwa katika Mji wa Blantyre nchini Malawi tarehe 14 Mei,
2014.
|
No comments:
Post a Comment