WANANCHI WANASUBIRIWA WATOE UAMUZI WAO: CCM YAFUNGA KAMPENI ZAKE KWA KISHINDO JIMBO LA CHALINZE - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Saturday, 5 April 2014

demo-image

WANANCHI WANASUBIRIWA WATOE UAMUZI WAO: CCM YAFUNGA KAMPENI ZAKE KWA KISHINDO JIMBO LA CHALINZE

MMG29677

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa Mkutano wa kufunga Kampeni za CCM,zilizofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze.
MMG29383
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,tayari kwa kufunga Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
MMG29338
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na Mkewe Bi. Arafa Kikwete wakiwapungia mikono wananchi wa Jimbo la Chalinze waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze wakiwasili  kwa ajili ya  kufunga Kampeni za CCM kwenye Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.
MMG29289
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,leo April 5,2014 tayari kwa kufunga kampeni za CCM.Kulia ni Mke wa Ridhiwani Kikwete,Bi. Arafa Kikwete.
MMG29404
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) na Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Dkt. Ali Mohamed Shein akibadilishana mawazo na Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete wakati wa kufunga Kampeni za CCM,zilizofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze.
MMG29423
Umati mkubwa wa wananchi wa Kijiji cha Kikaro,Kata ya Miono ndani ya Jimbo la Chalinze wakiwa wamefurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari ya Kikaro,Miono ndani ya Jimbo la Chalinze,leo tayari kwa kufunga kampeni za CCM.Picha zote na Othman Michuzi.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *