Waziri
wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu akizungumza na wanahabari wa
vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha juu ya kukamatwa kwa meno 53
ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7 na majangili sita
Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Sheluteteakifurahia jambo na wanahabari jijini Arusha
Wanahabari wa vyombo mbalimbali wakifatilia jambo kutoka kwa Waziri wa maliasili na utalii
Wizara
ya maliasili na utalii imetangaza kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye
jumla ya kilo 169.7na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu
pamoja na majangili sita katika wilaya ya manyoni mkoani Singida
Akitangaza
mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha jana Waziri wa maliasili na
utalii Mh.Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea jana katika
kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na
majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo
Waziri
Nyalandu alisema kuwa jumla ya majangili 6 wameshikiliwa chini ya
ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na
meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu
Nyalandu
alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili,
serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao
popote walipo huku akidai kuwa zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana
Aidha
alisema kuwa msako unaendelea kuwasaka wauwaji wa tembe 26,huku
akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao
kwa askari wa wanyamapori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama
Pia
alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyamapori na kikosi chake dhidi
ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa
weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na
meno ya tembo. Na Pamela Mollel wa Jamii Blog
No comments:
Post a Comment