MLIPUKO WATOKEA MITAA YA MIANZINI, JIJINI ARUSHA: KITU KINACHOSADIKIWA KAMA BOMU CHALIPUKA KATIKA BAR YA ARUSHA NIGHT PARK - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 14 April 2014

MLIPUKO WATOKEA MITAA YA MIANZINI, JIJINI ARUSHA: KITU KINACHOSADIKIWA KAMA BOMU CHALIPUKA KATIKA BAR YA ARUSHA NIGHT PARK

 Watu wakiwa katika hali ya taharuki mara baada ya kutokea kwa mlipuko wa kitu kinachosadikiwa kuwa bomu kilicholipuka katika bar ya "Arusha Night Park"  Maarufu kama (MTK) iliopo mianzini, jijini Arusha majira ya saa mbili kasoro usiku wa Jumapili.

watu wakichungulia eneo la ndani ya bar ya Arusha Night Park (MTK) ambamo mlipuko wa kitu kinachosadikiwa ni bomu lilipolipuka majira ya saa mbili kasoro usiku wa jumapili.

Blogu ya Wazalendo 25 Blog ilifika katika eneo la tukio majira ya saa mbili na nusu usiku , na kukuta watu wakiwa katika taharuki na wengine kuzimia mara baada ya kusikia mlipuko wa kitu kinachosadikiwa ni bomu.

Mlipuko huo ulitokea ndani ya bar hiyo,ambamo kuna nafasi ya wazi yenye kuruhusu watu kupata huduma, muda huo watu walikuwa wakitizama mpira wa miguu katika runinga ndipo walisikia kishindo cha mlipuko wa bomu hilo.

Shuhuda wa tukio hilo ambae hakutaka kutaja jina lake amedai kuwa mlipuko huo ulitokea hapo ndani wakati wakiangalia mpira na anahisi lilitegwa chini ya meza kwa kuwa hakuna nafasi ya kuruhusu kitu kurushwa kutoka nje, pia akaongeza kuwa"kwa kweli hakuna mtu aliekufa ila kuna watu zaidi ya wa tatu walioumia sana sehemu za miguuni na wengine wakiwa na majeraha mbali mbali" ,
Majeruhi walipelekwa katika hospitali ya Seliani na hospitali ya mkoa ya Mount. Meru zote za jijini Arusha.

Kwa habari zaidi endelea kutembelea Wazalendo 25 Blog.

No comments:

Post a Comment