Na mwandi wetu, Arusha
Naibu meya wa halmashauri ya jiji la Arusha Prosper Msofe pamoja na diwani wa kata ya kaloleni leo wamechezea kichapo kikali kilichowapelekea majeraha makali kutoka kwa mgambo wa jiji la Arusha.
Akiongea na waandishi wa habari diwani wa kata ya Kaloleni Ephata Nanyaro alisema kuwa tukio hilo la wao kupigwa limetokea majira ya asubui katika depoti ya manispaa ya jiji wakati walipoamua kwenda katika eneo hilo mara baada ya kusikia wananchi ambao ni wamachinga wakiwemo wamama wamekamatwa na kupelekwa katika depoti hiyo ya manispaa ya jiji huku wakiwa wanapigwa.
Diwani huyo alisema kuea naibu meya ameweza kupigwa sehemu mbalimbali za mwili ikiweo miguuu ambapo kwa upande wake yeye amueumizwa maeneo ya goti lake la kushoto ,mdomo pamoja na taya yake ya kushoto .
Aidha alibainisha kuwa wao kama madiwani walipewa taarifa leo asubui kuwa kuna wananchi waliopo soko kuu wanapigwa na askari mgambo wa jiji bila sababu yeyoyote ,huku akibainisha kuwa kisheria mgambo ao walikuwa hawatendi haki kwa jinsi waivyokuwa wanakamata watu kwani walikuwa hawafati sheria ya nchi ,bali walikuwa wanaenda kinyume na kanuni ya katiba ya nchi inasema usimpige mtu mara baada ya kumkamata bali umfikishe katika mikono ya sheria ikiwemo polisi.
Akielezea maelezo ya awali naibu meya Prosper Msofe alisema kuwa wao walipewa taarifa kutoka kwa baadhi ya wafanya biahara wadogo wadogo kuwa wanakamatwa na kupigwa pasipo sababu na vitu vyao vinachukuliwa hivyo ndipo walipoamua kuwafata mgombo hao katika depoti yao na walivyofika yeye kama naibu meya aliamua kuwaambia mgambo wale kwanini mnawapiga wananchi bure na sheria hairuhusu kupiga mtu bali kumkamata ndipo magambo wale waliwageuzia kibao na kuanza kuwapiga wao.
“sisi tulivyofika pale niliamua kuwauliza vizuri mgambo wale kwanini mnawapiga wananchi mara baada ya kuwakamata badala ya kuwachukulia sheria ya kuwapeleka polisi na sio kuwaweka huku depo basi mgambao wale ambao waikuwa zaidi ya 15 hawakuongea kitu bali walituambaia tu nyie ndo mnajidai madiwani wenyeviere here na kuwamua kuanza kutushambulia”alisema msofe
Alisema kuwa kufuataia tatizo hilo la wanachi kupigwa mara kwa mara mpaka sasa wananchi zaidi ya watatu wameshavunjwa miguu huku wengine zaidi ya sitini wameshapigwa favu na viboko na kati yao ,kunabaadhi yao ambao wame lazwa katika hospitali ya mkoa ya mounti meru wakiwa wanatibiwa na halmashauri ambapo alibainisha kuwa pia wananchi hao waliopigwa na kulazwa pindi watakapo pon a wanampango wa kuwafikisha mgambo hao mahakamani kusiana na matukio hayo ya kuwapiga.
Akiongelea tukio hilo meya wa jiji la Arusha Gaudence Lyimo alisema kuwa wao kama madiwani na meya wa jiji amepokea kwa masikitiko makubwa tukio hilo na alibainisha kuwa walichofanya mgambo hao wamekiuka sheria bali alisema kuwa wamekaa kikao cha muda na wameamua kuwasimamisha kazi mgambo wote kwa kitendo cha kuwazalilisha madiwani hao .
Alibainisha kuwa katika kipindi hicho ambacho madiwani hao wamesimamishwa kazi wataunda kamati ya uchunguzi ambao itawashirikisha baadhi ya madiwani pamoja na watendaji wa halimashauri ili kujua na ni anamakosa kati ya madiwani na mgambo na iwapo itagundulika ni mgambo basi watawachukuli hatua za kisheria.
Wakimweleza Mwandishi wa Habari kuwa tumepigwa na Mgambo wa Jiji kwasababu ya kutetea Uonevu na Udhalilishaji Unaofanywa na Migambo yoa wa Jiji kwa wananchi na wafanyabiashara ndogondogo. |
Siamini kama Wafanyakazi wangu wanaweza nishambulia kiasi hili |
Mh Kessy Diwani wa Kaloleni alikuwepo kuwapa joto madiwani wenzake |
Chriss akiongoza Makamanda kusubiri mpaka kieleweke |
Tutakomaa hapa Mpaka kieleweke |
No comments:
Post a Comment